Kunawakati nishawahi kueleza kuwa kama huna hoja ya maana ni afadhali unyamaze mpaka utakapopata kitu cha maana ndiyo uwasilishe. Mimi binafsi sina kadi ya chama chochote hivyo silazimiki kupepesa macho na kujaribu kutetea chama chochote, siamini kuwa ccm ni kibaya kiasi hicho, ccm sio mashine ccm inaongozwa na watu ambao watu hao wako ndani ya jamii tunayoishi, siamini na sitalazimishwa kuamini kuwa vyama vingine vina jipya zaidi ya ccm, ingekuwa nchi inaongozwa kwa mashine na kuwa vyama hivyo vinamashine zenye ziada ya kiufundi kuliko ccm ningeelewa, sioni jipya kwenye nchi za Africa zaidi ya wanasiasa kutafuta mbinu za kuwahadaa wananchi ili kupewa ridhaa ya kuongoza dola. sio siri ccm imefanya mengi tena makubwa, ni aibu kwa watu, au wanasiasa kujaribu kutamka kuwa hakuna lolote ccm imefanya, hizi ni chuki na niabu ya wazi kwa watoa hoja. Sioni kosa la Lusekelo kutetea chama chenye historia, Vyama vingine vyote hivi hata ofisi ni utata pamoja na kupewa mafungu makubwa ya kuendesha vyama. Sioni jipya. Kwa mimi itanichukuwa muda mrefu sana kuharibiwa ufahamu wangu kuwa ccm inatatizo kubwa, ni kweli kuna mambo ya kurekebisha ila kwa sasa hakuna kama ccm.