Akiongea machache kanisani kwake leo hii kwenye maombi ya kumwombea raisi na nchi mpya katika ibaada iliyofurika watu mbalimbali wakiwemo baadhi ya mawaziri au wawakikishi wao na baadhi ya wabunge walioenda kupata baraka za maombi mch Gwajima alisema.
"Ni kweli mikono ni ile ile, miguu ni ile ile na vidole ni vile vile lakini ikumbukwe kichwa ni tofauti. Ufanisi wa uwezo wa viungo vya mwili unategemea kichwa kilichopo."
Akaongeza pia
"Mabehewa yanaweza kuwa yale yale na Reli ile ile lakini kichwa cha Treni ni kipya. Speed ya mabehewa inategemea uwezo wa kichwa"
"Tumsuport Raisi kwa KAZI yake nzuri, ni mapema kulaumu na kushutumu, maendeleo hayaji kwa kubweteka na kulaumu. Kila mtu afanye kazi halali kwa bidii sana. Serikali inayo jali raia wake ni rahisi kwa raia hao kufanikiwa . Asiye na shamba atafute shamba sasa na serikali iweke mazingira bora kwa wananchi wake"