Mbwete abeza vyuo vya bweni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbwete abeza vyuo vya bweni

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 31, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Mbwete abeza vyuo vya bweni


  Na Charles Mwakipesile, Mbeya

  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria nchini, Prof. Tolly Mbwete ameishangaa na kuibeza mikakati ya serikali kuhusu kujenga vyuo vikuu vya bweni kila kanda kwa kuwa mpango huo ni kupoteza mabilioni ya Watanzania bila faida.Akizungumza wakati
  wa sherehe ya kuwapongeza wahitimu wa chuo hicho, Tawi la Mbeya katika ngazi ya cheti, shahada na shahada ya uzamili, Prof. Mbwete alisema kuwa inashangaza kuona wakati dunia kwa sasa inaweka mkazo katika vyuo vikuu huria, Tanzania inataka vyuo vya bweni.

  "Mimi nasema wazi ndio maana viongozi wa serikali tena wakuu wanashindwa kutambua mchango mkubwa chuo chetu ambacho ndicho kinachoongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi waliodahiriwa wakiwemo viongozi wengi,"alisema Prof. Mbwete.

  Alisema kuwa katika ulimwengu wa sasa Watanzania wanapaswa wapatiwe elimu huru itakayowawezesha kupata nafasi ya kusoma bila kuharibu ratiba zao na hivyo mpango wa kujenga vyuo vikuu vya bweni unaonesha jinsi ambavyo serikali iko tayari kupoteza mabilioni ya fedha bila huruma.

  Prof. Mbwete alisema kuwa mabilioni ya fedha yaliyotumika kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma yangetumika kujenga vyuo vikuu huria vingi ambavyo vingesaidia Watanzania wengi waliokosa nafasi kwenye vyuo vyuo vikuu vya bweni.

  Aidha Prof. Mbwete aliitaka serikali kutambua juhudi zinazofanywa na chuo hicho wakati wote inapozungumzia hali halisi ya elimu ya juu Alisema chuo hicho kimekuwa kikisahaulika na viongozi hao huku wakiujua kuwa ndicho chuo kikuu pekee kinachofanya kazi nzuri nchini.

  Alisema kuwa chuo hicho kimepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa na mwaka huu wamedahiri zaidi ya wanachuo 40,000 idadi ambayo ni ya juu kutokana na mwamko mkubwa wa Watanzania kupenda kukitumia chuo hicho.

  Alisema kutokana na mafanikio wanatoa huduma katika kanda nyingi na sasa wameanunua eneo la wazi karibu wakiwa na mpangoo kujenga Hotel ya Kisasa kwa ajili ya kitega uchumi.
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  analosema ni kweli, lakini akumbuke kuwa hata hizo nchi zilizoendelea bado wanatumia na kujenga mabweni sanjali na vyuo huria . Kuna masomo ambayo ni lazima uishi chuoni sababu ya ulazima wa masomo yenyewe kama udakatari ,engineer etc ,huwezi ukasomea nyumbani au distance learning wakati mda mwingi unatakiwa kuwa na wagonjwa ,lab ,reseach au mambo yanayolingana nayo. Course zingine kama za ujasiliamali ,Tourism etc sio lazima sana kuwa campus kwani hata ukiwa offcampus bado unaweza tu kumduu
   
 3. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ushindani wa kibiashara na pesa bwana! humfanya mtu afanye mambo ya ajabu hata kujidhalilisha, tumuulize yeye mpaka amfikia kuitwa Dokta alisomea shule ya kukaa kwa baba yake wapi sijui huko! Utakuta tangu darasa la 4 mpaka chuo kasoma bweni! Nyumbani kuna mazingira gani ya kusoma ktk Tanzania hii, mazingira kila kona baa, noise pollution, hakuna library mitaani, watu wasomee wapi, wanafunzi wake tunajua wanafanyaje mitihani na mazoezi mengineyo hatusemi, they really have no time kweli, wala conducive environment, asijipigie debe ili apate ulaji na kuporomosha elimu
   
Loading...