Mbwembwe za Mh Mulugo kwenye shule za wenzake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbwembwe za Mh Mulugo kwenye shule za wenzake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjenda Chilo, May 2, 2012.

 1. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Nimeangalia taarifa ya hbr TBC, Naibu waziri wa elimu kakusanya waandishi wa hbr na kwenda kuifunga shule kongwe ya binafsi Central sec pale Dom. Eti haina mwalim wa taaluma mara wa nidhamu na eti meneja wa shule sio mwalimu na pia eti walimu wengi wanaofundisha hapo ni part time.
  my take: Akaanze kufunga shule za serikali zenye mwalim huyo huyo ndo headmaster, taaluma, vifaa, michezo, muhasibu nk. Maisha bwana, wakati mawaziri wengine wamebandika plate no za stk badala ya W au NW wengine wako busy na waandishi ili waonekane wasitoswe kwenye cabinet mpya. kazi kweli kweli.
   
 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mpenda sifa sana huyu. Haitapita wiki wataifungulia tu.
   
 3. m

  massai JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  huyo mulugo kafoji jina mpaka vyeti,hana lolote huyo
   
 4. engineerm

  engineerm Senior Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jf bwana waziri akiwa mchapa kazi mnaanza kumpiga madongo tena akiwa mzembe anapigwa tena madongo sasa sijui tuamini lipi.by the way mi nadhani Mulungo anapiga sana kazi hadi amemfunika waziri mhusika,kama vp apewe tu uwaziri kamili wa wizara ya elimu.
   
 5. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Anajiita "Mzee wa kufunga" shule.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna uvivu mkubwa sana wa kufikiri huko serikalini. Unafungaje shule ghafla bila kutoa alternative kwa watoto walio darasani? Tunaambiwa hii shule ni kongwe, je, unafunga halafu watoto waende wapi? Kwa nini waziri asitoe muda kwa uongozi wa shule kurekebisha mambo na kama hilo halikufanyika ndio hatua nyingine zifuate?

  Na kama ubora ni tatizo huyu Mulugo anaweza kusema shule za kata zina ubora gani? Na kwa nini bado zipo?
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  well said bro!
   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kabla hajabomoa kwa wengine abomoe kwanza kwake
  hivi shule za kata ambazo zina mwalimu mmoja tu hazioni?
  hazina vifaa vya maabara na mahitaji mengineyo
  nadhani huyu anajiharibia sifa kwani uozo huo huko shule za serikali mbona hazifungi?
  labda kwa hili anadhani JK atampendelea ampe wizara kama kiongozi,akamuulize mwenzio mwantumu yu wapi
   
 9. M

  Mr.kibulala Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umesema neno,hyu jamaa ovyo kweli,aanze shle za kata kwanza,kama kuna shule itabaki.Hizo ni mbwembwe za kifala
   
 10. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani anapaswa kufanya utafiti na kupata ukweli kuhusu changamoto zinazozikabili shule zetu, hiyo ni sehemu ndogo sana, lakini shule za Serikali ndiyo zenye matatizo makubwa.
   
 11. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Mh. Mulugo anapiga kazi kuliko hata waziri wake!!! mbona ya Magufuli hamsemi akiwa anabomoa waliojenga hifadhi ya roads? shule zilizidi kuibuka bila mipango mtu anakurupuka anaanzisha shule mwisho wa siku vijana wanashindwa kufanya mitihani kisa usajili!! shule zingine hazifundishi walimu wake wanashiriki kuiba mitihani ili shule yake ionekane bora..Mwacheni naibu afanye kazi yake
   
 12. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nimeambiwa suala la kuifungia Central ni fitna kati ya rafiki yake-mwenye Martin Luther na mmiliki wa Central -mwl. Kigala. Mchezo ni huu; Luther ni kama shule ya kata, ina jina kubwa lakini darasa limerundika wanafunz, hivyo kumfanya mwanafunzi atoke kapa darasani. Wazazi wakigundua wanawatoa watoto wao na kuwapeleka central... Kwa kuwa mwenye Luther ni mshikaji wa Mulugo akamwambia Kigala, utaona! Na kweli sasa anaona. Wakuu wafuatilie sakata hili watafute ukweli, siyo kumwachia Mulugo aingize ushikaji kwenye kazi. Nawasilisha
   
 13. K

  KUTATABHETAKULE JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 807
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 80
  Wanadodoma tufahamisheni. Je Martin Luther ni shule ya Sekondari au la?
   
 14. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ulogi wa huyu naibu waziri ni balaa,haipiti muda mrefu ni lazima aende mashewa na maji marefu,hivyo ayatendayo ni strategies ndani ya defencing mechanism tu.mali alizo nazo ni za mashaka.mipango yake hufanya kama el[taasisi za dini].kifupi si mtu mwenye naksh nzuri katika 'virgin jobs'.
   
 15. M

  Malolella JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mkuu mmiliki wa Martin Luther ni nani?
   
 16. M

  Malolella JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni pre and primary school.
   
 17. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Anapiga kazi zipi? Huko kufungia shule za wenzake ndo unaita kupiga kazi, hizo sio kazi zake ni kazi za afisaelimu mkaguzi wa kanda mi nadhani jamaa hajui majukumu yake au anapenda coverage
   
 18. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kazi zake za Mwisho...atakaye kuja ataifungulia!
   
 19. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh "NW" loh;
  Bandugu mwenye kuweza kutuwekea overall results za skuli hii hapa tafadhari namuomba afanye hivyo"
   
 20. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Huyo Waziri aende shule ya Kibiti,hakuna waalimu A-level hasa sayansi na waalimu wanaotumika ni wa part time,kama ana courage afunge michepuo ya sayansi hapo Kibiti kwani ni waste of resource and time.
   
Loading...