Mbwa wa iringa wapoteza imani na binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbwa wa iringa wapoteza imani na binadamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 29, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Mbwa wa Iringa wapoteza urafiki Send to a friend FRM MWANANCHIWednesday, 29 September 2010 09:41 0diggsdigg

  Tumaini Msowoya, Iringa

  ZAIDI ya watu 250 wamejeruhiwa kwa kuumwa na mbwa kati ya mwezi Januari na Septemba mwaka huu, katika Manispaa ya Iringa kwenye matukio mbalimbali.

  Ilielezwa kwamba moja ya sababu ni tabia ya wafugaji wa mbwa kuwaacha wanyama hao wakizurura mitaani kinyume cha sheria.

  Akizungumza katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya kichaa cha mbwa duniani, daktari wa mifugo katika manispaa hiyo, Nikolas Mgumba alisema watu wengi wamekuwa waking’atwa na mbwa hao kutokana na wafugaji kutokuwa makini na mbwa wao, jambo ambalo ni hatari.

  Alisema mbwa wengi wamekuwa wakizurura kutokana na ukweli kwamba wanaowahudumia mbwa hao ni vijana wadogo ambao muda mwingi huwa shuleni.

  Alisema kutokana na hali hiyo, Manispaa ya Iringa kupitia idara ya kilimo na mifugo imefanya msako na kuwaua mbwa 36 wanaozurura mitaani.
  Akizungumzia chanjo, alisema kuwa manispaa hiyo yenye mbwa 2,758 ilichanja mbwa 1,694 ambao ni sawa na asilimia 61, huku asilimia 39 wakiwa hawajachanjwa jambo ambalo ni hatari.

  Alisema jitihada kubwa za manispaa hiyo ni kuhakikisha mbwa wote wanachanjwa sambamba na kutunga sheria zitakazowabana wamilikiwa wa mbwa kuhakikisha wanachanja mbwa wao.

  Hata hivyo aliwashauri watu wanaong’atwa na wanyama hao kutoa taarifa haraka kupata huduma ya haraka ya kukamuliwa damu katika eneo lililong’atwa ikiwa ni pamoja na kuosha kwa maji safi yenye sabuni, ili kupunguza sumu ikiwa mbwa aliyemng’ata ana kichaa.
   
 2. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa hao mbwa wanakosa imani vipi na binadamu? Hata sijakuelewa mkubwa hebu badili kichwa cha habari.
   
Loading...