Mvumbo
JF-Expert Member
- Aug 20, 2015
- 3,485
- 12,107
Mara baada ya kuona nyumbani mambo ni shaghala baghala kila mwenye lake hutenda, kila mwenye uhitaji huchukua, kila mtu anafanya atakavyo hivyo tukaona tuweke mbwa mkali na yote yatakoma.
Mbwa alizidi ukali kiasi kwamba hata ukipita mtaa wa pili anabweka! huna kosa anataka akung'ate! Aliharibu kwa wageni mpaka wazawa wa nyumba ile akidhani ndio usimamizi na ukali wake ndiyo mafanikio tuliyoyataka.
Akaona nyumba ni yake na tuliomuweka hatufai tena na hakutaka kutuelewa hata kwa ishara, hakika ikawa vigumu hata kwenda chooni.
Lakini, nawahusia watu wa nyumba yetu, tusimuogope maana bora athari ya kutokumuogopa kuliko athari ya kumuogopa kwani akifanya kila atakalo ni hatari kwa akili zake hizi.
Tusimame imara na kusema HAIKUBALIKI