Habari kama hizi Mimi pia nimekuwa nikizisikia.
Hizi ni miongoni wa taarifa ambazo huwa tunarithishana Vizazi na Vizazi bila hata kuwiwa kutafuta ni nini haswa kinatokea....utasikia Mtu anakuhadithia habari za Vibwengo, ukimuuliza umewahi kuwaona anakwambia amehadithiwa...na utatafuta mpaka uchoke hutompata aliyewahi kukutana na hao Vibwengo.
Nadhani Mchangiaji mmoja hapo katoa maelezo mazuri ambayo walau yanadhihirisha kuwa kuna Watu wamefanya utafiti na kujua kinachomkuta Mbwa, na si Mbwa tu bali Wanyama wengi wenye tabia ya kudadisi.
Na kama anavyoelezea Mchangiaji hapo Mimi kwa upande wangu nilitafuta taarifa nikakuta ni kwamba Mbwa huvutiwa na harufu inayotoka kwa Chatu, hivyo inapelekea kumsogelea akidhani inaweza kuwa ni chakula...Pia ukumbuke kuwa Nyoka wengi wana uwezo wa kutulia sehemu moja bila kujitikisa tofauti na viumbe wengine walivyo, maana hata namna yao ya kujilinda hufanyika wakiwa wametulia sehemu moja...hivyo ni rahisi kumvutia Mnyama Mwingine hata kama sio Mbwa kushawishika kumsogelea kujiridhisha kama yule ni Kiumbe hai au ni Mzoga.
Na si kwamba Chatu atammeza tu Kiumbe wake ghafla, la hasha Chatu hulazimika "kumkwida" Kiumbe husika mpaka atakapojiridhisha kuwa sasa anaweza kumeza bila Kiumbe husika kujitetea...na hawezi kufanya hivyo mpaka awe karibu na Windo lake, kwa Windo lenyewe kumkaribia au Yeye kumkaribia...na rahisi kwake ni yeye kukaribiwa kuliko kufuata.