Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 766
- 1,536
Na Victor Richard..
Judy ni mbwa jike aliyeishi kati ya mwaka 1936 hadi Februari 17, 1950. Mbwa huyu alikuwa
akiishi melini katika meli za HMS Gnat na HMS Grasshopper ambazo zilitia nanga huko Yangtze kabla na wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia.
Alidhihirisha uwezo wake wa kusikia ndege za maadui zilizokuwa zikiwajia na kutoa ishara kwa wanamaji waliokuwapo.
Baada ya baadhi ya wanamaji kuhamishwa kutoka meli ya Gnat na kupelekwa katika meli ya Grasshopper mwaka 1939,meli ilipelekwa Singapore na hii ni baada ya Uingereza kuamua kuingia vitani dhidi ya Ujerumani.
Judy alikuwa melini wakati wa mapambano ya Singapore ambapo alikuwapo pia wakati Grasshopper ikiwahamisha wanamaji wake kuelekea Dutch East Indies lakini ikiwa njiani meli hiyo ilizama na Judy alikaribia kupoteza maisha kutokana na kunaswa na mlolongo wa makabati yaliyoanguka, hata hivyo aliokolewa na wanamaji waliorudi melini wakitafuta masalia.
Katika kisiwa hicho kikame akiwa na wanamaji waliosalimika,Judy aliweza kutafuta vyanzo
vya maji safi vilivyowasaidia wote. Baadae walifanya safari kuelekea Singkep,Dutch East India na kisha Sumatra kwa lengo la kutengeneza namna ya kuyaokoa majeshi ya Uingereza.
Baada ya safari ngumu iliyokatisha maili 200 za pori kwa wiki tano wakati ambapo pia Judy alinusurika kuuawa na mamba, wanamaji waliwasili siku moja baada ya meli ya mwisho kuondoka na hivyo kuangukia kwenye mikono ya wajapani na kufanywa wafungwa wa kivita, Judy akiwa miongoni mwa wafungwa hao.
Judy alihamishwa kinyemela na kupelekwa kambi ya Medan ambako alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi mwandamizi wa Jeshi la anga anayeitwa Frank Williams ambaye aliishi naye kwa kipindi chote kilichosalia cha maisha yake.
Williams alimshawishi Kamanda wa kikosi kumsajili Judy kama mfungwa wa kivita akipatiwa namba ‘81A Gloergoer Medan’.Judy alikuwa ni mbwa pekee aliyesajiliwa kama mfungwa wa kivita katika Vita kuu ya pili ya Dunia.
Judy alizunguuka katika kambi kadhaa,akisalimika/nusulika kifo baada ya meli ya mizigo ya SS Van Warwyck kuzama ambapo kipindi kifupi baadae aliweza kuwaokoa abiria katika meli iliyokuwa ikizama.
Les Searly kutoka katika meli ya Grasshopper ilimuiba tena Judy na kumpeleka katika kambi nyingine ambako aliungana tena na Frank Williams.
Baada ya Vita ya pili ya Dunia kuisha,maisha ya Judy yalikuwa hatarini kwa mara nyingine.
Alikaribia kuuawa na walinzi wa Kijapani kufuatia mlipuko wa chawa miongoni mwa wafungwa,hata hivyo Frank Williams
alimficha mbwa huyu hadi vikosi vya muungano vilipowasili.
Searly,Williams na wengine walimchukua Judy kinyemela hadi Uingereza na alitumia miezi sita akiwa katika Karantini.
Judy alitunukiwa medali ya Dickin na PDSA na alikufa mwaka 1950 nchini Tanzania wilayani NACHINGWEA mkoani Lindi kutokana na tatizo la seli baada ya kusafiri na Frank Williams katika Skimu ya Karanga.
Medali na kola ya Judy vimehifadhiwa katika jumba la makumbusho liitwalo Imperial War Museum lililoko Duxford kama sehemu ya kutambua mchango wa Mnyama katika vita
Maisha yake ya awali.
Judy alizaliwa mwezi Februari 1936 katika jengo la kuzalishia mbwa lililoko Shanghai China ambalo lilikuwa likitumiwa na wataalam wa Kiingereza kupata mbwa.
Judy alikuwa miongoni mwa watoto saba waliozaliwa kwa mama aliyeitwa Kelly ambaye ni kizazi cha mbwa waliotoka Sussex.
Akiwa na umri wa miezi mitatu,Judy alitoroka na alitunzwa na muuza duka hadi alipotimiza miezi sita.
Kufuatia mvutano kati ya wafanyakazi wa meli ya wanamaji wa kijapani,Judy mfanyakazi wa jumba la kuzalishia mbwa na alirudishwa katika jengo hilo.
Kwa asili mbwa huyu aliitwa Shudi jina ambalo KIANGALIKANA linajulikana kama Judy. Katika
kipindi ambacho Judy anarejeshwa, mzazi wake na ndugu zake hawakuwapo.
Katika msimu wa kipupwe wa mwaka 1936 wanamaji wa meli ya HMS Gnat waliazimia kupata nembo ya meli yao ambayo huwa ni mnyama ambae huwakilisha kundi, hii ni kutokana na meli shindani za HMS Bee, Cicada na Cricket kufanya hivyo.
Luteni Kamanda J. Waldergrave na Afisa Mkuu msaidizi Charles Jefferey walimnunua Judy kutoka katika makazi yao na kumjumuisha na kundi la wanamaji wa HMS Gnat.
Judy aliorodheshwa kama Judy Sussex
katika orodha ya Jeshi la Mfalme la wanamaji.
Lengo kuu ni kumfunza kutumia bunduki lakini
watu walianza kumtumia kama mbwa wa kawaida na siku kadhaa baada ya kuwasili
Jefferey alitangaza kuwa “Uwezekano wa kumfanya Judy kutumika Kivita ni mdogo mno, muda mwingi alioutumia mitaani Shanghai ulimfanya akose umahiri katika uwindaji, kazi pekee anayoweza hutumiwa ni kunusa vyakula....!!