Mbwa aliyetelekezwa baada ya mmiliki kufariki

Sabaya hii ajira isiyo rasmi uliyoianzisha hapa jf inakwenda kukuharibia kesi maana yapo mengi uliyoyafanyana wenzako yanaandikwa hapa ma wapelelezi wa kesi zako wanayachota kirahisi tu!
Hawa uliowaajiri hawakusafishi Bali wanazidi kukupaka oil chafu!
Pambana kimyakimya kujinasua na achana na hawa watetezi njaa!
 
Majiran= uv chchm😄😄😄😄 nimeikubali hii fasihi. Salute kwa mtoa uzi.
 
TUJIFUNZE KIDOGO HAPA KUHUSU HUYU MBWA
(Jeremiah kipoya)
Mwenye nyumba aliamua kufuga mbwa ili amsaidie kulinda mali zake nyumbani hasa nyakati za usiku
Akamfundisha yule mbwa kulinda nyumba na mbwa akawa mkali kweli yani ana bweka hata ukisogelea tu uzio wa nyumba anayolinda
Mwenye nyumba akampenda sana yule mbwa kwakua alikuwa anafanya kazi aliyo mfundisha pia wana familia wa nyumba hiyo walifurahi pia kwa utendaji wa yule mbwa
Majirani na wezi walimchukia sana yule mbwa kwakua kubweka kwake wao waliona ni kelele usiku anawasumbua wezi nao wakaona anawakosesha fursa ya kuiba mali za mwenye nyumba
Siku moja mwenye nyumba alifariki na hapo mambo yakaanza kuwa magumu kwa yule mbwa, Majirani na wezi walisema atakoma aliyemfuga na kumpa chakula kashaondoka sasa ngoja tumnyooshe huyu mbwa.Mbaya zaidi hata wanafamilia wa hiyo nyumba anayoilinda nao wakaanza kumuona huyo mbwa ni kero anawapigia kelele usiku na amezidi ukali na ukorofi
Wanafamilia wakajadili wamfanye nini huyo mbwa? Wamtupe mitaani? Wamuue? Wakaona hapana ni bora wamng'oe meno na kucha kwakua hata kuwa tena na nguvu ya kung'ata, atakuwa mnyonge na mwenye msongo wa mawazo yani hata kuwa na maana tena na hata piga kelele za kubweka
majirani na wezi wakafurahi sana kwakuwa kazi ya kumkomesha huyo mbwa imefanywa na wanafamilia wenyewe
Je nani wa kumtetea mbwa? Watu wote wamemgeukia?Amepewa hukumu nzito kwa kufanya kazi aliyo fundisha na aliye mnunua na kumfuga je tumlaumu marehemu mwenye nyumba?
UMEJIFUNZA NINI KWENYE HIKI KISA??
Jeremiah Kipoya
sema aliyechukua majukumu ya kuilea ile familia aligundua yule Mbwa alikuwa anakula vifaranga vya majirani.yaani alikuw tayari ameshakuwa mbwa kokoko kitambo
 
Back
Top Bottom