Mbwa aliyetelekezwa baada ya mmiliki kufariki

Hayanihusu lakini fasihi iliyotumika hapa ni ndogo sana......raha ya fasihi ifikirishe, sio sentensi ya kwanza tu tayari unakiona anachohangaika nacho mwandishi.
 
Tena ashukuru angekuwa huku kilolo tungemtengeza supu huyo mbwa.
Kala kuku wetu na vifaranga wengi tu
 
Nimejifunza kwamba mwenye mbwa alikuwa na wazimu kwa kufuga mbwa koko aliyechukiwa hata na wanafamilia sembuse wapita njia!!?.
 
Ukiona hivyo jua mbwa alikuwa anautii kwa mwenye mbwa tu, aling'ata hata wanafamilia au mbwa alikuwa kichaa, lakini mwenye mbwa peke yake alikuwa akimwona huyo mbwa ni mzima.
 
nimejifunza mbwa alikuwa mbwa koko,angekuwa mbwa mwenye discipline angependwa na kukubalika hata baada ya bwana wake kufariki
 
Tatizo la mbwa ni vile alijipa mamlaka hata ya kung'ata wapita njia.

Tena akawa anaenda mpaka nyumba za jirani kusumbua watu kwa vile tu tajiri yake anamlinda.

Sasa mbwa anakula jeuri yake.
 
Mbwa alifundishwa ujambazi, means mwenye nyumba nae alikuwa jambazi
 
Nimejifunza kuwa sabaya ni jambazi tu ila kuna mandezi wanamtetea. Acha mahakama ifanye kazi yake.
 
Kumtetea mbwa aliyekuwa anaumiza maisha ya watu haina maana.Naona waliokuwa wanafuga mbwa wanahangaika sana na walisahau maisha ya watu waliokuwa wanaumizwa na watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…