Mbuyu twite katua rasmi jangwani

MTUNZA AMANI

Senior Member
Jun 2, 2012
187
21
Hayawi hayawi yamekuwa,leo majira ya saa 10:15 kwa saa za afrika mashariki ilikuwa ni chereko nderemo na vifijo pale mashabiki wa Yanga walipojaa uwanja wa ndege wa Mwl Julius Kambarage Nyerere kumpokea mchezaji huyo wa Kimataifa. Hakika watu walijaa huku kelele za mashabiki zikisikika 'Twite Twite ,Twite' walijaa mlangoni hadi pale wasimamizi wa getini wakalazimika kumpitisha kupitia mlango wa watu mashuhuri. Mara baada ya kufika walimkabidhi jezi ya no 4 ya club ya yanga. Baada ya hapo Mbuyu Twite alipanda gari ndogo ya yanga huku msafara mkubwa ukiongozwa na pikipiki,magari na wengine kwa miguu. Msafara huo ulienda hadi msimbazi ukawaacha hoi mashabiki wa Simba,hawakuamini kile walichokiona, baada ya kufika Jangwani Twite alipanda gorofani na kuwasalimu wana yanga huku akiwaahidi kufanya mazuri Jangwani hapo na kuwaburudisha mashabiki.
NAWASILISHA.
 
Malizia,alivishwa jezi ya njano yenye maandishi RAGE mgongoni.
 
Back
Top Bottom