Mbunge Zungu: Tumeanzisha kodi ya miamala ya simu kwa watu milioni 30 wenye uwezo, waliobaki zaidi ya milioni 20 hawatalipa

"Ujerumani yenyewe imeweka solidarity fund hii ni kwa ajili ya wale wenye uwezo kutoa ili kuwasaidia wale wenye uwezo mdogo. Ukikatwa usijiwaze wewe, waza wale ambao wanahali ya chini kuliko wewe". - Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akitetea Tozo za miamala ya simu
 
Tusiwe kama dodoki, unapokopi kitu kutoka nchi fulani lazima ukopi na mazingira (supporting background/context) yake pia. Hapa kwetu unaongelea watu kma machinga wanaendesha bodaboda, wakulima wa kijembe cha mkono na kusubiria mvua bila kutumia pembejeo, wafugaji wa kuhamahama, wavuvi wanaovua kwa vyandarua vya mbu, wakulima wasiokuwa na soko la mazao yao, watu ambao wanajinunulia dawa kihola kwenye vijiduka vya dawa,
 
Zungu ungeleta na wazo jema la UB 40 (unemployed benefit) yaani malipo ya paundi arobaini kwa wasio na ajira, ningekupigia saluti.
 
Hivi huyo Zungu hajafa tu?
 
Huyo mwandishi angemuuliza mtu mwenye uwezo ni yupi? Mwenye simu? Anayatumia fedha [kiasi chochote?], Maana hii tozo hata kama unamtumia mtu hela ya matibabu ambaye hana uwezo kiuchumi, yeye anakatwa na wewe unakatwa! CCM sijui wanatumia akili gani!
Kuna mwandishi wa habari Tanzania mwenye uwezo wa kuhoji? Yaani mwandishi anabakia kujichekesha tu hajui lolote nashindwa kuelewa ni kujipendekeza ili apate uteuzi au ni kitu gani?
 
Hajafa tu huyu fisadi wa kiafghanistani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…