Yakhe usitumie jazba, nilichoandika kuhusu zungu ndio ukweli wenyewe, wewe hujui kuwa kina Mo, walitaka kupewa hati ya Selander Bridge? hujui kuna viwanja vingapi vya wazi Dar es Salaam vilivyochukuliwa na wajanja? Dar es Salaam umekuja lini? kwa sisi tuliokuwepo miaka ya 70-80 hapo tunajua ni maeneo mangapi ya wazi sasa ni maeneo binafsi. Kama hufahamu jaribu kuuliza kwa wahusika upate taarifa zaidi.Maana hufahamu hapa JF anayeandika ni nani.ni vizuri ukagonga hodi kwenye ofisi zenye vile vibao vya ofisi ya ....,
Kukufikirisha tu kidogo, UDA iliyosababisha iddi Simba apande kwa pilato kujibu tuhuma ilikuwa chini ya nini hapo dar?wajanja kina sugar daddy wa zungu walifanyaje?kama hujui kinachoendelea dar, si vibaya ukaomba wazee wa ilala wakakufunda, kushinda kariakoo sio kujua kinachoendelea Ilala.
Kuhusu wamachinga, hili nin tatizo kwenye jamii, ni tatizo gumu, kulitatua kwa njia nyepesi sio njia sahihi ya kulitafutia ufumbuzi. Sidhani kama kuna serikali yenye akili timamu duniani, yenye kufurahia ongezeko la wamachinga mtaani. Serikali yenye akili hutafuta njia sahihi za kurasimisha hizi biashara ndogondogo, kwa kuwatafutia maeneo rasmi.
Tatizo la serikali yenu mnayoichagu ya CCM mara baada ya kurubuniwa na hao kina zungu ni kutokufikiria chanzo cha watu kuamua kuwa wamachinga. Wengi wanafanya hivyo kwa kukosa fursa za kueleweka kwenye maeneo ya uzalishaji, ajira rasmi n.kama ma-elfu wa wamachinga Dar wangekuwa mashambani japo mkuranga tu, nina imani hili lingekuwa jambo jema. Lakini hao kina Zungu mnaowachagua kila siku wanafurahia mkijazana hapo kkoo, kwa kuwa nyie ni daraja rahisi la kuwapa kura/kula.
Sio kila anayepingana na wewe kwenye jukwaa hili ni CCM au mfuasi wa CCM,wewe unakuwa na kuweweseka kama kwa CDM ambao kila mtu mwenye kuwaeleza mapungufu yao wanamwita katumwa na CCM au msaliti. Ni dalili ya kufikiria kwa kiwango cha chini sana.nakushauri punguza jazba fikiria, kama umekwama uliza.