dm2000inter
Member
- Oct 27, 2010
- 29
- 10
Ukisoma ile makala ya Mwanahalisi between line juu ya mtazamo wa Zambi utaona wazi kuwa Zambi yupo sahihi zaidi ya 100% hata kama huyu Eric anataka kutumia mahakama kumziba mdomo.Board ya kahawa wajumbe wake JK na Waziri wake wa Kilimo wamechemka kwenye uteuzi wa Board Members.Total Conflicts of interest between board members.
Tatizo ni Zambi ama alieteua Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi, halafu tatizo lipo wapi kwakuwa sasa ni soko huria
Mimi Sija soma hilo Gazeti lakini ukweli ni kwamba Kampuni ya Lima Kuendelea kununuakahawa Mbichi Yaani "Cherry" huu ni wizi, kwa sababu wananunua kwa Bei ndogo sana alafu hawana mpangowowote wa kufufua zao la kahawa zaidi ya kuwaibia wana mbozi Mimi naungana na Mh. Zambi katika hili la kuwapiga vita walanguzi wa zao la kahawa katika Wilaya yetu ya Mbozi Na kwingineko.
Mkuu usitutukane watu wa Mbozi kana kwamba sisi tutachagua kumwuzia kahawa yetu Lima anayetupunja. Wewe na Zambi wako tuacheni soko lituamlie wapi tuuze kahawa yetu kuliko kutulazimisha tuwauzie waswahili wanaochukua kahawa yetu kwa kutukopa kutulipa inakuwa taabu.
Nimesoma articles mbili kuhusiana na hii saga. Mwanahilisi na Mwananchi. Yangu mimi ni maswali mawili tu:
1. Kwa nini Lima wananunua kahawa mbichi (cherry)?
2. Uteuzi wa Board unazingatia nini?
Mbona sioni tatizo la hiyo kauli, kama kweli wanafanya haki na siyo dhuluma kwa nini waogope? hapo lazima kuna ulaghai wanafanya na hivyo wameona wameumbuliwa.
Halafu siku hizi bana Tanzania hizi kesi za kupuuzi zimezidi eti kesi 2.4 bill, yaani mtu anajitamkia tu kiasi cha fedha anachotaka. Hii laana imetoka wapi? Lengo nini kama siyo kutaka kuwanyamazisha watu wasikemee maovu kwa kuogopa kesi za billions?
Ee Mungu iokowe nchi yangu niipendayo ya Tanzania, na mikono ya wanyanganyi hawa wasio hata na huruma wala haya.