Mbunge wako ni wa aina gani?

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Baadhi ya Wabunge wetu ni wazuri sana. Huchangia na kusimamia hoja za msingi za kutetea maslahi ya watu wa Jimbo lake na Taifa kwa ujumla.

Wabunge wengine huenda Bungeni kusinzia, kukaa tu kimya au kuchangia hoja za kulinda maslahi yao tu.

Je, Mbunge wako ni wa aina gani?
 
Mchapakazi sana sema hayupo kwenye wezi wa taifa hili maana hao ndio wananchi Sasa

USSR
 
Baadhi ya Wabunge wetu ni wazuri sana. Huchangia na kusimamia hoja za msingi za kutetea maslahi ya watu wa Jimbo lake na Taifa kwa ujumla.

Wabunge wengine huenda Bungeni kusinzia, kukaa tu kimya au kuchangia hoja za kulinda maslahi yao tu.
Je, Mbunge wako ni wa aina gani?
Mbunge wangu mimi ni kama huyu anayepeleka hoja kama hizi bungeni.

20220411_130026.jpg
 
Mbunge wangu, Jerry Slaa, hakuna alichofanya kwa miaka hii miwili tangu aingie kazini. Kila kitu kimekufa, barabara hazijakarabatiwa mpaka zimegeuka mahandaki na hata maji yamesitishwa kusambazwa.

Ukonga jimbo lipo wazi kwa miaka miwili sasa. Tunaiomba Tume ya uchaguzi iitishe uchaguzi mpya mapema iwezekanavyo ili kujaza pengo la huyu mtu.
 
Baadhi ya Wabunge wetu ni wazuri sana. Huchangia na kusimamia hoja za msingi za kutetea maslahi ya watu wa Jimbo lake na Taifa kwa ujumla.

Wabunge wengine huenda Bungeni kusinzia, kukaa tu kimya au kuchangia hoja za kulinda maslahi yao tu.
Je, Mbunge wako ni wa aina gani?
Sijui kama kuna watu wana wabunge kwenye hilo genge la wahuni waliopora haki ya wananchi kuwachagua wabunge wanaowataka.

Mtu ambaye angeweza kusema kama alichokuwa amepanga kukipata katika huo uchafu, kama amekipata au la, kwa bahati mbaya hayupo Duniani.
 
Mbunge wangu anatuhuma kabla hajawa mbunge yaani ghasia tu alimuradi ni mbunge
 
jimbo langu tangu nazaliwa yeye ni wakupita bila kupingwa.

halafu mjivuni
 
Mimi Sina mbunge. Kuna kimemo kilitoka kwa Bashir kwamba namba moja na mbili wakatwe Kisha mkurugenzi akaambiwa amtangaze namba tatu awe Kama mbunge.
Bashir mwenyewe kawa Kama huyo aliyempendekeza, wote hawasikiki bungeni
 
Back
Top Bottom