Mbunge wako ametimiza wajibu wake?

Mbunge wako ametimiza wajibu wake?

donimuya

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2011
Posts
272
Reaction score
55
KAZI ZA MBUNGE

1) Kuwawakilisha wananchi
2) Kutunga sheria
3) Kuisimamia Serikali


MBUNGE WAKO AMEFANYA HIVYO

Mimi kwangu Morogoro mjini. Wana morogoro tujiulize je ABOOD ametuwakilisha vizuri BUNGENI na kwenye vikao vya MADIWANI kwa kuchangia kutunga sheria nzuri zitakazotetea maslahi ya wananchi wa morogoro na kuzisimamia?

Je ameisimamia serikali kuhakikisha inatekeleza wajibu wake kwa wananchi? kwa mfano amefanya nini kuhakikisha VIWANDA haviuzwi kifisadi? au na yeye amekuwa sehemu ya wizi huo?

RUSHWA NA UFISADI mahospitalini, polisi, mahakamani, TRA na kwenye ofisi mbalimbali za umma, ABOOD ametuwakilishaje katika kukemea hilo? au ametumia nafasi hii ya ubunge kukwepa kodi, kujipatia mali zetu na kuziua?

MAJI yalikuwa yakipatikana karibu siku nzima baadhi ya maeneo, sasa imekuwa ya mgawo. ametuteteaje kwa kuibana serikali kuhakikisha maji yanapatikana kama zamani na kuongeza huduma ya maji ya bomba maeneo yasiyokuwa na maji?

ABOOD amefanya nini katika kuisimamia serikali ili itupatie huduma bora? mfano huduma za AFYA je amesiimamiaje serikali kutekeleza ahadi ya wazee kutibiwa bure na madawa kupatikana bila mizengwe?

Amesimamiaje upatikanaji wa ELIMU BORA na sio bora elimu katika shule zetu za kata?

Je amefanya nini kuhakikisha serikali inatutatulia kero zetu? mfano migogoro ya ardhi (mashamba na viwanja), unyanyasaji viwandani na wafanyakazi kulipwa mishahara midogo, au na yeye amekuwa sehemu ya unyanyasaji huo?

Amesimamiaje michango ya wazazi katika shule za kata kuhakikisha inatumika kwa kazi iliyokusudiwa au anatazama tu zikiliwa na wajanja wachache?

NADHANI HAJAFANYA KAZI ZA MBUNGE ipasavyo, kazi alizofanya (mfano kutoa bus la kuzikia au kusaidia vikoba kina mama) ni kama za kina Mengi, Manji, Bakharesa nk, ambapo lengo lao huwa ni kulinda maslahi binafsi.

TUNATAKA MBUNGE, anayejuwa kazi za mbunge na azitekeleze kwa vitendo, VIJANA wenye sifa kutoka chama chochote jitokezeni kugombea nafasi hii,

WANANCHI WA MOROGORO tuonyeshe mfano kwa kuonyesha kuwa tuna uelewa na siyo jinsi mikoa mingine wanavyotuchukulia. eti mara abood au shabib au sadiki nk.

MUNGU IBARIKI MOROGORO
na naamini mikoa mingine mtatutendea haki katika uchaguzi huu kwa kutuletea wabunge wenye sifa sahihi MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Tatzo Lao Hawana Maamuzi Kwa Serikali Yao, Hawana Uwezo Wa Kushauri Na Kusimamia Serikali, Na Hii Ni Kutokana Mfumo Uliopo Kwny Serikali. Wanaambiwa Waunge Mkono Tu Hata Kama Jambo Lenyewe Lina Madhara. Tunapaswa Kuzidi Kuwaombea Viongozi Wetu ili kuharibu iyo mifumo
 
wabunge wa upinzani kwa kiasi fulani wamejitaidi kufanya kazi zao kibunge ipasavyo. ila upande wa ccm ni wachache sana wametimiza wajibu wao kama kina esther bulaya,kangi lugola,filikunjombe,Ally kessy,hamis kigwangallah na hata Ruhaga mpina. pia bila kumsahau peter serukamba. waliobaki wa ccm ni shida walituangusha.
 
Mbunge wangu Lema, hakuna alichofanya Arusha zaidi ya kutuletea vurugu zilizokimbiza watalii na kurudisha nyuma uchumi wa Arusha. Kitu pekee alichofanya ni kujenga gorofa lake Njiro
 
Mbunge wangu Lema, hakuna alichofanya Arusha zaidi ya kutuletea vurugu zilizokimbiza watalii na kurudisha nyuma uchumi wa Arusha. Kitu pekee alichofanya ni kujenga gorofa lake Njiro

Fanya kazi, acha kulalamika utakufa maskini.....
 
Mbunge wangu~ Lazaro nyalandu huyu anatuleteaga wasanii tu hakuna anachofanya jimboni ! Barabara kiwango cha vumbi alafu imechibuka balaa!! Hii ndo sgda jimbo La kaskazin
 
Mbunge wangu Lema, hakuna alichofanya Arusha zaidi ya kutuletea vurugu zilizokimbiza watalii na kurudisha nyuma uchumi wa Arusha. Kitu pekee alichofanya ni kujenga gorofa lake Njiro
mkuu hilo gorofa lake linakunyima usingizi kabisa,kwa siku unalitaja si chini ya mara 20!! Achana nalo mkuu,litakuua kwa presha bure,fanya kazi kwa bidii,panga mipango yako vizuri,hamisha makazi, kutoka huku jf na ukapige kazi,utajenga gorofa hata wewe,pia punguza husuda
 
Mimi Mbunge wangu ni Halima Mdee, naona yeye hana mpango wa kugombea mara ya pili, toka ameingia sidhani kama hii Halmashauri imefanya lolote lile
 
mbunge wangu ni sitta!!! hastahili kabisa ametukosea heshima mpaka amechakachua katiba ya wananchi na kufuata watu wachache ..
 
Stephen Wasira ametimiza majukumu yake vizuri Jimbo la Bunda.
 
Mbunge wangu Hawa Ghasia kazi za kibunge huwa hafanyi mala nyingi anasafiri kwenda India kumfuata mumewe, huyu mama anastahili kupunguziwa majukumu, hata kijijini kwake IMEKUWA hajawawakilisha vizuri 90% hawana vyoo wanajisaidia baharini
 
Duuu kijana wangu Mnyika ; Maji yako shingoni aidha azame au aibuke.
 
Haya ndiyo mambo ya msingi sana kwetu wananchi kujadili sio kupoteza muda kwa ushabiki wa vyama,ushabiki wetu wa vyama uliyopitiliza ndiyo unaowafanya hata hao wabunge kusahau kazi zao.
 
Mimi Mbunge wangu ni Halima Mdee, naona yeye hana mpango wa kugombea mara ya pili, toka ameingia sidhani kama hii Halmashauri imefanya lolote lile

Halima amefanya vzr,ila tumpe madiwani wa kutosha
 
Halima amefanya vzr,ila tumpe madiwani wa kutosha

Wewe waishi wapi labda? Maeneo niishiyo toka amekuwa mbunge sijaona chochote kimefanywa na halimashauri ya kinondoni ambayo yeye ni mhusika humo ndani.
Kuanzia mikocheni B hadi target barabara ni ile ile
 
Mbunge wangu yeye ni ubabe tu hana lolote la maendeleo,nani mbunge pekee aliyefanikiwa kuwagawa wapiga kura wake kwa asilimia kubwa!
 
Mbunge wangu mnyika han lolote alilolifanya zaidi y kuomba miongozo ambayo haitusaidii wana ubungo.

Barabara za mitaani tabu kwa mfano ya makoka ubungo wakati huu haifai kabisa, manispaa ilitoa milioni 370 ameshindwa kusimamia matokeo yake barabara haina mitaro basi, imekuwa kero, alituahidi maji lakini mpaka leoakina swai wanaendelea kutuuzia maji dumu sh. 1000.
Ukuend mbezi msakuzi hawajawahi hata kumuona, kuna tabu ya daraja ktk awamu ya watu 14 wamesombwa na maji ktk mto mpiji wakiwamo watoto. Kuna mtu kajitolea makaravati mbunge haponekani, mashuleni ndio tabu kabisa. Yaani najutia kura yangu kwa chadema na mnyika
 
Mbunge Wang Makongoro mahanga hakuna alichofanya kinachosikitisha hatukumchagua sisi hasa wakazi wa Tabata kimanga.
 
Back
Top Bottom