Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe ajivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga CCM

Endelea kuota, Chadema ni taasisi imara na inazidi kua imara sasaivi ili uwamini jaribuni friend match tu bila police na tume ilio huru japo ya muda tu, You will thank me later

Sent using Jamii Forums mobile app
Taasis imara inategemea makapi ya ccm! Taasis imara gani haina uwezo wa kuandaa makada wake badala yake inaamini mpinzani wa kweli ni yule anayetoka ccm na siyo ndani ya taasis yenyewe!
 
CECIL MWAMBE ATANGAZA KUACHANA NA CHADEMA NA KUOMBA KUJIUNGA NA CCM
View attachment 1358493
'Kuanzia leo Februari 15, 2020 ninajivua Ubunge wangu na nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA, na nimeamua kujiunga na CCM' - Cecil Mwambe aliyekuwa Mbunge wa Ndanda
Huyu hapa
 

Attachments

  • Kabla ya Msaliti Sumaye na Mwambe kurudi kwao walikotokea Ccm sikiliza hawa Maka ( 352 X 640 ).mp4
    2.1 MB
King Ngwaba,
Na hicho ndicho kinachotakiwa na siyo michezo ya kubadili gia angani. Leo chadema inajidhalilisha kwa kumuomba mpinzani wao mwenyekiti wa CCM akubali maridhiano na matokeo yake akina Sabaya na Polepole wanawajibu wafanye hayo maridhiano ndani ya chama chao kwanza au sharti kwanza wakubaliane na sera za CCM!
 
Polepole alisema mwisho wa usajili ni mwaka jana. Sasa mbona wamefungua dirishsha dogo tena. Au ndio zile hela za jumuiya ya Ulaya zimeanza kutumika?

Haya nendeni Arusha mkammalizie Bananfa na yule diwani mwenzie. Hawa hata mkiwapa laki tano tano watakubali tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la wanachama wa Chadema wengi bado hawajui mzizi wa tatizo la wabunge wa Chadema kujivua ubunge na kurudi CCM.

Sisi ambao hatuna upande wowote tuliwashauri mkaanza kutukana matusi na matokeo yake ndiyo hayo sasa. Tatizo liko kwa mwenyekiti wenu na lilianzia wakati wa uchaguzi uliopita hasa baada ya kuanza kuwachukua wanachama walioshindwa kura za maoni kutoka CCM na kuwafanya kuwa wagombea wa Chadema kwa nia ya kuogeza ruzuku bila kuangalia athari huko mbeleni.

Tuliwaambia tangia mapema msichukue makapi kutoka CCM badala yake tuliambulia matusi. Mlitaka kujenga ghorofa kwa siku moja na mkasahau wahenga walishasema "Tamaa ilimponza mzee fisi".
 
Informer,
Maajabu ya Tanzania mtu anagombea wenyekiti wa Chama halafu baada ya mwezi eti mawazo yake ni tofauti😂😂.

Je unaamini sera gani halafu wanatoa sababu za kibinafsi ambazo sijasikia watu wamehama CCM kwa sababu hizo. Ni bora watu wachache makini kuliko wengi ambao hawana tija
 
Hata wanao mpokea nao, hamnazo. Mtu katoka Mwanza kwenda Dar na CHADEMA BUS, kafika Chalinze eti analemka na kutafuta usafiri mwingine na kutoa kashfa kwa hilo gari lililomfikisha hapo! Angetelemkia Misungwi au Shinyanga. Sidhani kama CCM watampa nafasi ya kugombea Ubunge. Angepoteza kitu kwanza kwa hatua hiyo, ndipo angeonekana ni kweli ana mapenzi na CCM. Kwa sasa anataka kuifanya CCM kuwa daraja kwake!
Hivi ni CHADEMA ndo ilimsaidia Mwambe au Mwambe aliisaidia CHADEMA? Kabla ya Mwabe CHADEMA iliwahi kuwa na Mbunge Lindi au Mtwara?
 
Na chadema wakayapokea "majizi" hayo kwa gharama ya kubadili gia angani na kumpoteza katibu mkuu wao Slaa na matusi na kejeli kwa mwenyekiti mwenza wa ukawa, Lipumba.


Baadae tena yale Majizi na Mafisadi Papa kama Lowassa, Sumaye, Rostam na mchukia ufisadi Dr Slaa wakarejea CCM.
 
Informer, Naiona CHADEMA mpya, kwa hakika chujio kali lilitumika kuchuja makapi na mapandikizi ndani ya uongozi wao wa kitaifa.

Hakika hiki ni chama makini na imara, ila kisirudie makosa yake ya kuwakaribisha wanachama wanyemelea vyeo toka vyama vingine hasa CCM na kuwaacha kuwaamini makada waandamizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afadhari amehama labda bei ya simenti itapungua bei na sisi walalahoi tujenge nyumba.
 
Back
Top Bottom