Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe ajivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga CCM

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Kuna tetesi kuwa Mbunge Cecil Mwambe wa CHADEMA atatimkia CCM wakati wowote weekend hii.

Kuna mtu ana undani wa taarifa hizi?

------Update-----

CECIL MWAMBE ATANGAZA KUACHANA NA CHADEMA NA KUOMBA KUJIUNGA NA CCM
2307852_IMG_20200215_151307.jpg

'Kuanzia leo Februari 15, 2020 ninajivua Ubunge wangu na nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA, na nimeamua kujiunga na CCM' - Cecil Mwambe aliyekuwa Mbunge wa Ndanda.

Katika Uchaguzi mkuu uliofanyika 2015,Cecil Mwambe akiiwakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215.

7 Oktoba 2019 akiwa Mtwara, Cecil Mwambe alitangaza kuwania uenyekiti wa CHADEMA taifa. 19 Desemba 2019 Matokeo yalipotangazwa, Bwana Cecil Mwambe alipata Kura 59 sawa na asilimia 6.2, huku Mshindani wake Freeman Aikael Mbowe akipata kura 886, sawa na asilimia 93.5.
 
CECIL MWAMBE ATANGAZA KUACHANA NA CHADEMA NA KUOMBA KUJIUNGA NA CCM
IMG_20200215_151307.jpg

'Kuanzia leo Februari 15, 2020 ninajivua Ubunge wangu na nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA, na nimeamua kujiunga na CCM' - Cecil Mwambe aliyekuwa Mbunge wa Ndanda
 
Back
Top Bottom