Mbunge Wa Muda Mrefu Kusimamia Uchaguzi Wa Spika

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,280
307
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Bunge kwa vyombo vya habari ni kwamba uchaguzi wa uspika utafanyika Alhamis wiki hii na utafanyika chini wa usimamizi wa mbunge mwenye muda mrefu kuliko wote bungeni.
Kuna uwezekano mkubwa Edward Lowassa kuusimamia unless kama kuna mbunge mwingine, Je kama Andrew Chenge akipitishwa kugombea na kwa sababu yeye yuko against demokrasia ndani ya bunge na ameahidi kutoruhusu mijadala dhidi mafisadi na chama tawala ambayo kwa mtazamo wake inadharirisha na kuchafua viongozi na watu mbalimbali, pia kufanya chama tawala kushindwa kupitisha mipango ya utekelezaji sera zake.
Kwa Lowassa kusimamia si itkuwa rahisi Chenge kushinda na kulifanya bunge bubu
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,730

Let them dig their own grave !!!!!!!
 
Dina

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
3,165
1,691
Huo ndio utaratibu wa siku zote? Hawa watu wakoje jamani?
 
Najijua

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,039
179
mbona huyo katibu wa bunge hamtaji huyo mbunge wa siku nyingi ni nani?kwani si ameshawajua wabunge wote au kama kawaida yao wanataka kufanya funika kombe mwanaharamu apite?
 
Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Sep 8, 2010
1,017
256
mbona huyo katibu wa bunge hamtaji huyo mbunge wa siku nyingi ni nani?kwani si ameshawajua wabunge wote au kama kawaida yao wanataka kufanya funika kombe mwanaharamu apite?

miongoni mwa wabunge wa muda mrefu bungeni - Anna Abdallah na Anna Makinda na wote ni wagombea.
 
3D.

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,013
280
Mbunge mwenye muda mrefu zaidi ni Anne Makinda, tangu 1975 yuko bungeni ila kwa kuwa ni mgombea ni wazi kuwa hatosimamia.
 
boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,280
307
Mbunge mwenye muda mrefu zaidi ni Anne Makinda, tangu 1975 yuko bungeni ila kwa kuwa ni mgombea ni wazi kuwa hatosimamia.

Ni kweli Anna Makinda ni wa muda mrefu pia lakini kwa kuwa anagombea utaratibu wa bunge hautamruhusu, halafupamoja na kwamba Anna abdalla anagombea nafasi ya uspika lakini si mbunge hivyo yeye tayari hawezi kusimamia.
Unless kama kuna mbunge mwingine mbali na Lowassa, nina hofu sana kama kesho CC ya CCM ikimpitisha Chenge kesho katika majina matatu moja kwa moja kutakuwa na njama za kumweka Chenge badala ya Sitta
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom