Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nafuatilia Bunge la 11, Mkutano wa 2, Kikao cha 6 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge wanachangia mjadala Mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa unaokusudiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2016/17.
Pamoja na mambo mengine, Julius Kalanga ameipongeza Serikali kwa kupeleka fedha za kuendeshea shule wilayani kwake kwa wakati na zinazokidhi haja. Ameiomba Serikali kuendelea kupeleka fedha hizo ili kuboresha elimu yetu. Aidha, mbunge huyo ametaka kuwe na mjadala wa kitaifa juu ya mfumo wa elimu nchini badala ya kuacha jukumu hilo mikononi mwa wanasiasa. Kwamba ametaka mjadala huo uhusishe wataalam wa elimu na hasa Walimu ambao wana uelewa mpana juu ya elimu yetu. Amesema kuwa mjadala huo utaondoa uwezekano wa mawaziri wanaopewa dhamana ya kusimamia elimu kuichezea Elimu yetu. Amempongeza Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako kwa kurejesha mfumo wa Division