Mbunge wa Mbeya mjini apata ajali, mtoto afariki

Taarifa iliyorushwa hivi punde na kituo cha ITV kupitia kipindi chake cha habari zilizotufikia hivi punde zinasema Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu mbunge Wa Mbeya mjini amenusurika kifo baada ya gari lake kufeli bleki na kumgonga mtoto wa miaka 15 aitwae Rachel ambapo mtoto alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitali.

Mh. Sugu alikuwa akielekea uwanja wa ndege Songwe ndipo alipo fika maeeneo ya Iyunga akapata ajali hiyo mbaya japo yeye na dereva wake hawajapata madhara yeyote mpaka gari hilo lilipo weza kusimama eneo la Tazara Mbeya.

Aidha gari la polisi lilolokuwa likienda kutoa msaada eneo la ajali hiyo ya Mh. Sugu nalo limepata ajali na kupinduka huku askari wake wanne Kati ya sita waliokuwepo wakijeruhiwa.

Tunatoa pole kwa ndugu Wa mtoto, Askari waliopata ajali wakitimiza wajibu wao na Mh. Mbunge wa Mbeya mjini.
Poleni wote mliopatwa na matatizo.
 
Sugu nae apunguze ushirikina...mwaka jana gari lake lilipata ajali Kitonga leo limeua......Haya maagano na waganga wa kienyeji hayafai
Kwa kua wewe ni mwandani wake basi unajua siri nyingi zaidi
 
Sugu nae apunguze ushirikina...mwaka jana gari lake lilipata ajali Kitonga leo limeua......Haya maagano na waganga wa kienyeji hayafai
Tanzania ni nchi insyoongoza Kwa kuamini ushirikina. Watu wa aina yako ndio wanaoipaisha nchi yetu juu kwa kuamini ushirikina. Kila siku ajali zinatokea acha kuaibisha nchi.
 
Sugu nae apunguze ushirikina...mwaka jana gari lake lilipata ajali Kitonga leo limeua......Haya maagano na waganga wa kienyeji hayafai
Mawazo potofu kama haya hayafai hata nikipewa hicho kichwa bure sipokei.
 
Taarifa iliyorushwa hivi punde na kituo cha ITV kupitia kipindi chake cha habari zilizotufikia hivi punde zinasema Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu mbunge Wa Mbeya mjini amenusurika kifo baada ya gari lake kufeli bleki na kumgonga mtoto wa miaka 15 aitwae Rachel ambapo mtoto alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitali.

Mh. Sugu alikuwa akielekea uwanja wa ndege Songwe ndipo alipo fika maeeneo ya Iyunga akapata ajali hiyo mbaya japo yeye na dereva wake hawajapata madhara yeyote mpaka gari hilo lilipo weza kusimama eneo la Tazara Mbeya.

Aidha gari la polisi lilolokuwa likienda kutoa msaada eneo la ajali hiyo ya Mh. Sugu nalo limepata ajali na kupinduka huku askari wake wanne Kati ya sita waliokuwepo wakijeruhiwa.

Tunatoa pole kwa ndugu Wa mtoto, Askari waliopata ajali wakitimiza wajibu wao na Mh. Mbunge wa Mbeya mjini.

Poleni wahanga wote.

Natumaini Mh. Sugu ameahirisha safari, kusimamia maafa haya.

Asijiite Rais wa Mbeya bila kuwa responsible..

Time will tell...
 
Uzembe wa dereva, hiyo gari ni scania ya upepo? Usijaribu kudanganya umma. UMEUA. Hakuna SUV hata saloon zinafeli brake 1.5km! Mechanical mechanism ya brakes miaka hii sio ile ya zamani.
taratibu mkuu
 
Back
Top Bottom