Mbunge wa jimbo la Kondoa kaskazini aweka jimbo mfukoni

Mbunge wa jimbo la Kondoa kaskazini aweka jimbo mfukoni

mapambanodaima

Senior Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
108
Reaction score
15
Wanajamvi katika hali ambayo ni ya kusikitisha mbunge huyu Zaben Muhita hajawahi kuonekana jimbon kwake zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa.Wakati huo wanainchi wakikabiliwa na matatizo lukuki kama maji,barabara na hata njaa kali sana ambayo inawatafuna ndugu zangu.

Mbunge huyu alipewa dhamana hiyo tangu 2005 lakin hakuna chochote alichokifanya jimbon mpaka hivi sasa na ameliweka jimbo mfukon kwa maana ya kwamba ameona jimbo ni lake daima. Niwashauri warangi wabadilike huyu mama hana lolote tuangalie mtu atakayetusaidia kutuletea maendeleo.

Kwanza huyu mama hajawahi kuzungumzia tatizo sugu la maji bungeni na hata barabara,nawasilisha
 
Mkoa wa Dodoma kwa ujumla hauna wabunge wachapa kazi wengi ni mburura mburura!
 
kiukweli inakera kweli kweli na hii ni kutokana na tatizo la elimu kwa ndugu zangu pia na kujisahau kwa wale waliobahatika kupata elimu mapema na kushindwa kulipa fadhila kwa ndugu zao. tunamifano mingi sana ya viongozi ambao hawana habari na wilaya yao. jamani tujitokeze kuijenga Kondoa yetu tutabaki na historia ya michoro ya mapangoni tu.
 
Katika wilaya zilizonyuma kimaendeleo nchini ni pamoja kondoa.huyu mama ni useless tatizo ni la warangi wa kuendekeza ukabila na udini...even Nkamia hana anachokifanya.2015 inakuja nadhani mabadiliko yanatakiwa wa mkoa mzima wa Dodoma
 
Kondoa ina tatizo kubwa kuliko inavyoonekana. Kondoa ni moja ya njia zinazotumiwa na ccm kula fedha za Watanzania. Hivi ni wilaya gani hapa Tanzania ambayo haina jengo la polisi? Ni Kondoa, jengo ambalo polisi wanatumi lilikuwa msikiti wa Waarabu wakati wa biashara ya utumwa. Tangu hapo Tanzania haijafanya kitu.
Kinachoangusha zaidi watu wa Kondoa ni udini na elimu ndogo. Mfano miaka ya themanini jamaa moja anaitwa Magingi aligombea ubunge Kondoa, akishindana na Nyanganyi, lakini Nyanganyi kwa sababu ya dini alipita. Magingi alikuwa na elimu na uwezo wa uongozi lakini hakupata nafasi. Mwaka 2010 vijana walijitokeza kugombea ubunge, wakiwemo Sanda, Mresa, Moni na nyanganyi akiwemo. Lakini kwa vile Zabeni alitoa mikeka kule Busi, Pahi na sehemu nyingine alipita. Bila kusaidia mikeka au kujenga misikiti hupatu ubunge. Hii ni aibu kwa Kondoa. Tunao wasomi wengi ambao wangeweza kusaidia Kondoa lakini kwa vile ni "Wakristo" wao wenyewe wanajua kufanya hivyo ni kupigia mstari jibu. Ni kwamba hawatachaguliwa. Mfano, tunao watu waliowahi kushika vitengo vikubwa, lakini hawaoti hata kwenda Kondoa kwa sababu wanafahamu kwamba ni kupoteza mda.
Hata hivyo kuna uwezekana mkubwa sana Zabeni akaendelea na ubunge wake hata mwaka 2015-2020 kwa sababu watu ni wale wale na akili ni zile zile. Kondoa inatia simanzi kwa sababu watu wake wamelishwa matango pori. Maendeleo Kondoa ni ndoto kwa sababu watu wananunulika kirahisi mno. Mfano mzuri ni Nkamia. Tofauti na vijana wenzake bungeni yeye amekuwa kimya. Hakuna asemacho, hakuna kinachoendelea, kama si mbunge wa Ilemela aliyesema ataweka shilingi kupinga bajeti wizara ya Ujenzi mwaka 2009 hata sasa kusingekuwa na chochote kinachoendelea.
Kondoa ipo nyuma sana na hii ni kutokana na jinsi walivyo, wanakera na fanatics zao za kidini. Kwa njia hii wanakosa viongozi shupavu na wenye maono ya mbele.
 
Wanajamvi katika hali ambayo ni ya kusikitisha mbunge huyu Zaben Muhita hajawahi kuonekana jimbon kwake zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa.Wakati huo wanainchi wakikabiliwa na matatizo lukuki kama maji,barabara na hata njaa kali sana ambayo inawatafuna ndugu zangu. Mbunge huyu alipewa dhamana hiyo tangu 2005 lakin hakuna chochote alichokifanya jimbon mpaka hivi sasa na ameliweka jimbo mfukon kwa maana ya kwamba ameona jimbo ni lake daima. Niwashauri warangi wabadilike huyu mama hana lolote tuangalie mtu atakayetusaidia kutuletea maendeleo. Kwanza huyu mama hajawahi kuzungumzia tatizo sugu la maji bungeni na hata barabara,nawasilisha
Mama anajua silaha yake kubwa ni udini na pesa maana wakristo wapo 5% ya population ya Kondoa. Kwa hiyo mama kajichimbia anatafuta pesa akija atakuta warangi wachache wamekufa njaa waliobaki atawaokoa halafu kura kama kawa. Mama Kamua wajinga ndyo waliwao wanauliza maji wewe ndiyo kisima?
 
Warangi ni wanafiki.... Walichagua udini, sasa wacha wale mafi yao
 
Waziri w Maafa wa Bunge la kwanza aliloliunda JK mwaka 2005.Kweli Huyu mama ni Maafa.
 
adui mkubwa wa kondoa ni ukristo , uchaguzi iliopita ijumaa ya mwisho kabla ya uchaguzi ilitembea kampeni misikitini eti wakristo walioomba kuchaguliwa kupitia ccm ilisemekana walitumwa na wanafadhiwa na askofu na mkristo akichaguliwa kuwa mbunge atajenga kanisa kila kijiji
 
Kondoa iko nyuma kimaendeleo lakin tuache unafiki huyu mama kawasogeza kidogo haswa kwenye suala la maji na barabara visima kadhaa vimechimbwa na barabara zimechongwa na atleast zinapitika karibu mwaka mzima jimbo lile lina kata 28 2010 alishinda kata 24 na aliingia 2005 sasa mtu ambaye haonekani jimbon angeshinda kwa kiasi hicho na alimshinda mpinzani wake kwa zaidi ya kura 10,000 bado mnasema ooh hajafanya lolote na hili la udini inakuaje maana mpinzani wake mkuu alitoka cuf nae alikua muislam pia,acheni siasa za majitaka!
 
kondoa ni tatizo sana hasa vijijini wananchi wengi ni wa hali ya chini sana njaa inawamaliza..
 
Mnamtaka arudi jimboni kwake kwenda kufanya nini, ilhali alishamalizana na wapiga kura wake wakati wa uchaguzi? Hivi ukinunua kitu (let say baiskeli) kutoka kwa mtu mkamaliza biashara kwa maana ya kubadilishana fedha kwa baiskeli, utalazimika kurudi kwa aliyekuuzia baiskeli kufanya nini tena? Umesikia anataka kuuza baiskeli nyingine? Huyu mbunge aliwahonga pesa, wali, khanga, kapelo, chumvi na t-shirt Warangi wakampa kura. Huo ndio ulikuwa mwisho wa biashara. Anatakiwa arudi tena huko kama kuna uchaguzi mwingine i.e. 2015. Na pia wale wote waliomchagua hawana haki ya kumdai chochote au atekeleze ahadi yoyote kwakuwa alishawapa vitu (pilau, chumvi, kapelo, khanga n.k.) ambavyo wao wapiga kura waliviona vitawafaa kwa miaka 5 kuanzia mwaka 2010. Tuwe fair. Warangi tulieni bana. Mliamua mlichokiamua kwamba thamani yenu ya miaka 5 ni chumvi pakti 1, ubwabwa wa shughuli, kapelo, t-shirt, na vgcent kidogo.
 
Ok'nimekusoma kama mdau wa jimbo la kondoa suala kubwa ni kutoa elimu ya uraia kwa warangi ili makosa waliyofanya yasijitokeze,vile vile tuhamasishane ili kuachana na mazoea ya kumchagua mtu ambaye hafanyi chochote
 
Arudi kufanya nini alichaguliwa ili atumikie nyani mitin au atumikie wapiga kura wake? hogo za t shirt kapelo hazimfanyi asirud jimbon mie ni wa huko ila 2015 nafikiria kwenda kumtoa nipen ushirikiano hafanyi kitu yule mama anayesema katengenez barabara nani wapi kachimba visima? aliyefanya kazi kwa mda mfup watu wakaona faida ya kumchagua ni NKAMIA tu.
 
Kondoa ina tatizo kubwa kuliko inavyoonekana. Kondoa ni moja ya njia zinazotumiwa na ccm kula fedha za Watanzania. Hivi ni wilaya gani hapa Tanzania ambayo haina jengo la polisi? Ni Kondoa, jengo ambalo polisi wanatumi lilikuwa msikiti wa Waarabu wakati wa biashara ya utumwa. Tangu hapo Tanzania haijafanya kitu.
Kinachoangusha zaidi watu wa Kondoa ni udini na elimu ndogo. Mfano miaka ya themanini jamaa moja anaitwa Magingi aligombea ubunge Kondoa, akishindana na Nyanganyi, lakini Nyanganyi kwa sababu ya dini alipita. Magingi alikuwa na elimu na uwezo wa uongozi lakini hakupata nafasi. Mwaka 2010 vijana walijitokeza kugombea ubunge, wakiwemo Sanda, Mresa, Moni na nyanganyi akiwemo. Lakini kwa vile Zabeni alitoa mikeka kule Busi, Pahi na sehemu nyingine alipita. Bila kusaidia mikeka au kujenga misikiti hupatu ubunge. Hii ni aibu kwa Kondoa. Tunao wasomi wengi ambao wangeweza kusaidia Kondoa lakini kwa vile ni "Wakristo" wao wenyewe wanajua kufanya hivyo ni kupigia mstari jibu. Ni kwamba hawatachaguliwa. Mfano, tunao watu waliowahi kushika vitengo vikubwa, lakini hawaoti hata kwenda Kondoa kwa sababu wanafahamu kwamba ni kupoteza mda.
Hata hivyo kuna uwezekana mkubwa sana Zabeni akaendelea na ubunge wake hata mwaka 2015-2020 kwa sababu watu ni wale wale na akili ni zile zile. Kondoa inatia simanzi kwa sababu watu wake wamelishwa matango pori. Maendeleo Kondoa ni ndoto kwa sababu watu wananunulika kirahisi mno. Mfano mzuri ni Nkamia. Tofauti na vijana wenzake bungeni yeye amekuwa kimya. Hakuna asemacho, hakuna kinachoendelea, kama si mbunge wa Ilemela aliyesema ataweka shilingi kupinga bajeti wizara ya Ujenzi mwaka 2009 hata sasa kusingekuwa na chochote kinachoendelea.
Kondoa ipo nyuma sana na hii ni kutokana na jinsi walivyo, wanakera na fanatics zao za kidini. Kwa njia hii wanakosa viongozi shupavu na wenye maono ya mbele.
naona unabwabwaja kwelikweli. unaonaje ukahamia jimbo lingine. maana tanzania kubwa, unaweza kwenda hata karatu, kuliko kukaa hapo ukisononeka kwa watu waliotumia demokrasia yao.
 
Yeah kuna dalili kubwa ya zabein kuendelea na ubunge 2015 coz anapga kazi na wananchi wanaiona we endelea na propaganda zako humu jf eti ameshinda kwa udini wakati hata aliyeshika nafasi ya pili na mpinzani wake mkuu pia alikua muislam sasa udini unakujaje naona unatapatapa
 
Back
Top Bottom