Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh. Wilfred M. Lwakatare akanusha kushikiliwa na jeshi la polisi.

Alex Xavery

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
230
196
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh.Wilfred Lwakatare akanusha kushikiliwa na jeshi la polis.

Kufuatia taarifa zinazoendelea kusambaa katika jamii kuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh.Wilfred Lwakatare anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuandika barua kwa ajili ya kuomba misaada ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lilotokea septemba 10 mwaka huu mkoani Kagera,tayari amelitolea ufafanuzi.

Mh.Lwakatare amesema kuwa yeye hajashikiliwa na jeshi la polisi na leo ni siku ya tatu yupo Dodoma katika vikao vya kamati za Bunge kwa sababu ni mjumbe wa kamati ya nishati na madini,pili amesema kuwa alienda polisi kwa ajili ya kutoa maelezo ya ziada kwa jambo lililokuwa limeleta utata dhidi ya kijana mfanyabiashara katika manispaa ya Bukoba maarufu kwa jina la Edison Fashion ambaye alikuwa anamuuzia vifaa vya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi ambaye ndo alikuwa ameshikiliwa kwa ajili ya kutoa maelezo.

Aidha amesema kuwa baaada ya serikali kusema wataanza na taasisisi muhimu za kijamii,aliamua kuomba misaada kwa wadau wake kuwaelekeza kuwa atakayekuwa tayari kuchangia alipe moja kwa moja kwa mwenye duka ambapo yeye atakuwa anaenda na kamati yake kuchukua vifaa na kuwasambazia waathirika hao,na hali hiyo ndo ilipelekea kijana huyo kushikiliwa na jeshi la polisi.

Pia mh.Lwakatare amesema kuwa baada ya kufika polisi na kutoa maelezo ya kujitosheleza,jeshi la polisi lilimuachia Bw.Edison bila mashariti yoyote nayeye nay eye aliruhusiwa siku hiyo hiyo na kuanza safari ya kuelekea Dodoma,huku akisema kuwa hakuna fedha yoyote iliyokuwa imeshachangwa na mpango wake ulikuwa bado haujaanza kazi badala yake kuna fedha walichanga yeye pamoja na wabunge wawili wenzake kiasi cha shilingi milioni moja laki nane na elfu arobain {Tsh.1,84,000/=} ambazo alinunua turubali kwa ajili ya mahema na mashuka {blanketi}na vyote wameshaaanza kuvigawa kwa wananchi wa jimbo lake la Bukoba mjini.

SAUTI YA MBUNGE LWAKATARE
 
Back
Top Bottom