WanaJF,
Juzi Mbunge wa Ileje mh. Kibona alitoa mpya, stori ambayo mpaka sasa imeacha maswali mengi na watu wakianza kuhoji elimu na uwezo wa Mbunge huyo.
Mbunge huyo alipoombwa kutoa kusalimia kwenye Mkutano wa Bulembo alidai anasikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya makada wanaotoa misaada wilayani humo. Alimtaja mh. Janet Mbene N/w/fedha kuwa anafanya hivyo kupitia viongozi wa chama wilaya na kata.
Wananchi walimzomea Mbunge huyo ambaye tangu amekuwa Mbunge anakaa Rungwe na hajafanya chochote tangu amekuwa Mbunge.
Wamedai yeye amekuwa anagawa chumvi, mananasi, nguo, unga n.k vitu ambavyo havikuwa kwenye ahadi zake wakati anagombe.
Wananchi wamedai Mbunge huyo ni mzigo kwa CCM na serikali yake. Wamesema kila anapoitwa kutatua matatizo ya jamii amekuwa akitoa ahadi bila kuzitekeleza. Pia wamedai ametelekeza familia ya Katibu wake aliyefariki.
Hata hivyo kiongozi mmoja wa CCM alisema misaada anayotoa Mbene inawasaidia sana wao kama chama kutekeleza ilani ya CCM kwani anawasaidia mambo mengi.
Hata hivyo katibu wa Siasa wa Mh, Mbene akihojiwa kwa simu na radio Mbeya FM juu ya madai hayo, amesema wao wanafanya kazi Maeneo Mengi Tanzania wanapoombwa kufanya hivyo. Amesema kauli ya Mbunge ni kuwafedhuri wananchi ambao walikuwa na shida nyingi na sasa wanapunguziwa.
Amesema Mbunge anapaswa kuwaomba radhi wananchi ambao amewatukana.