Mbunge wa cuf na posho, taarifa rasmi za bunge (hansard)

ithangaledi

Member
Jun 4, 2011
84
57
Katika pitapita kwenye taarifa rasmi za Bunge nilikutana na kituko cha mbunge wa cuf akilalamika kuchelewesha posho zao;

Mheshimiwa Spika, la mwisho, Kamati mbili tofauti, kuna Kamati ya Uongozi ya Bunge ambayo ni Wenyeviti na Makatibu wetu wa Kamati na kuna Kamati hii Councilors. Wenyeviti wanatusaidia maslahi yetu kwenye Kamati… SPIKA: Unamaanisha Commission?


MHE. MUSSA HAJI KOMBO: Naam! SPIKA: Unamaanisha Commission? Commission ya Bunge, hii ya pili? Ya kwanza Kamati ya Uongozi ambayo ni Wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu na kama Mwenyekiti hayupo basi Makamu Mwenyekiti anakuwepo. Nyingine ni Tume ya Bunge sijui ndiyo ipi unayoisemea? (Makofi) MHE. MUSSA HAJI KOMBO: Nashukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunisaidia, kwa sababu nilijua utanisaidia kwa sababu na wewe uko ndani yake. (Makofi) Mheshimiwa Spika, sisi Wabunge maisha yetu yanakwenda na Tume hii na siyo kitu cha kufanyia mchezo ndani ya Bunge letu. Wabunge wanaoishi hapa Dodoma wanaishi katika maisha magumu sana. Tunasikitika sana Tume yetu ya Wabunge yenye nia njema ya kusaidia Wabunge wetu eti inashindwa kutekeleza kwa sababu mtu mmoja kasema hatutaki mafao, hatutaki hivi, sisi sote Wabunge tufe na njaa, tupate matatizo. Hatuwezi! Nakusudia kusema kwamba sisi tumeunda Tume yetu kwa maslahi yetu na wote hawa waliokataa, waliokubali, walipiga kura kwa maslahi ya Tume hiyo. Tunakwama, juzi tulichelewa kutiliwa posho katika Benki ya CRDB, jana tumetoka mie, Mheshimiwa Sanya, nanyi mpaka benki ya CRDB kwenda kufanya ghasia angalau tusiaibike. (Kicheko) Mheshimiwa Spika, sasa tunakaa, tuna maslahi yetu, tuna Tume yetu ambayo haingiliwi na Serikali. Ni Tume ya Bunge inaangalia maslahi yetu. Halafu haitekelezi matakwa yetu kwa sababu eti mtu kakataa. Naomba Mheshimiwa Waziri ukija uniambie nini sababu yake. (Makofi/Kicheko) Mheshimiwa Spika, kwa sababu wakati wa kusali umefika na nimaliza kwa kusema nakushukuru sana Mheshimiwa Spika. (Kicheko/Makofi
 
Hadi leo<

Ni ziito pekee ndiye asiyechukua posho bungeni, wabunge wote wa chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao mbowe wanaendelea kuchukua posho kila kukicha.
 
Ndiye yy alisema wao wanaongozwa na msomi mbdiyo maana kila kitu wanaeam ndiyo mzee. Lakini chadema wanaongozwa na disco joka......
 
wanafanya kazi ya ziada angalau CUF isikike tena masikioni mwa watu
 
Back
Top Bottom