Mbunge wa CHADEMA aitaka serikali kuweka utaratibu maalum wa watu kutumia majina ya Waasisi wa Taifa

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Mbunge Leticia Nyerere (Viti Maalum-CHADEMA), amesema ni vyema serikali ikaweka utaratibu maalumu wa kutumia majina ya waasisi wa taifa na si kila mtu kulitumia hata katika dhihaka.
Alisema hivi sasa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia majina hayo kwa manufaa yao na wengine hata kuyatumia vibaya ikiwemo kuyafanyia dhihaka.

“Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya majina ya viongozi wetu na hata kuyafanyia dhihaka, lazima tuhakikishe suala hilo linakoma.

“Mimi ni mkwe wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, lakini inasikitisha unapoona baadhi ya watu wanatumia jina la kiongozi huyo kwa dhihaka, ni muhimu sasa kukawekwa sheria ya kuyalinda majina hayo,’’ alisema Leticia.

Wakati huo huo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye jimbo lake limekuwa kinara wa maandamano, jana alipinga hatua ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kuitaka serikali kuweka Sheria Maalum kudhibiti watu wanaofanya maandamano bila mpangilio.

Lema, ambaye muda wote alikuwa akijaribu kujenga hoja za kukataa ushauri huo wa Kamati ya Bunge, alisema maandamano si tukio la ghafla na kwamba, haliwezi kupangiwa siku wala muda wa kufanyika.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, maandamano ni kitendo cha ghafla, hivyo kukipangia siku na sehemu ya kupitia hayatakuwa maandamano bali ni mazoezi ya kupiga vita kisukari,’’ alisema Lema.

Awali, Mjumbe wa Kamati hiyo, Vita Kawawa, akiwasilisha taarifa hiyo bungeni, alisema umefika wakati kwa serikali kuwasilisha Muswada utakaoweka utaratibu wa watu ama vikundi kuandamana tofauti na ilivyo sasa, ambapo kila kukicha watu hupanga maandamano bila kujali athari za usalama na kiuchumi.

Kawawa, ambaye alisoma taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Edward Lowassa, alisema kwa sasa kuna vyama vya siasa vimekuwa vikiandama bila kuzingatia muda wala siku, hivyo kuleta usumbufu kwa watu wengine.
 

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
2,000
Kudhihaki watu wawe viongozi ama la ni jambo lisilo sahihi, ila pamoja na hilo, hivi ni nani aliyempa Mwalimu Nyerere Ubaba wa taifa?
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Hoja ya Mh. Leticia Nyerere ni hoja nzuri katika taswira ya nchi yetu.

Kama kuna uwezekano hata utawala wa Jamiiforums ungeweka utaratibu wa uhakiki zaidi wa watu wanaotaka kuwa verified member ambao wanakuja na majina ya waasisi wa taifa letu kwa nia ya kujisimika kitapeli katika uwanja wa hoja kwa manufaa yao.

Ni jambo la kushangaza sana unapomuona mtu anajiita na kujinasibisha kwa jina la ubini wa mwasisi wa taifa letu huku akidai hilo lilikuwa ni jina la Babu wa Babu yake au Baba wa Babu yake na wengine wanafika hatua yakudai hilo ni jina la ukoo wao na wengine hata kudiriki kusema wao ni watoto wa mmoja wa waasisi. Kwa kitupi hawa ni matapeli na wanasumbuliwa na inferiority complex katika utapeli wao kwenye jamii.

Wanaishi kwa kutumia nyota za binadamu wengine kwa maslahi yao binafsi. Lazima watu kama hawa wasipewe mianya na kuyafanya majina ya waasisi wa Taifa letu yaonekane yamebeba makokolo ya utapeli.

Kwenye hoja nyingine. Ni kweli maandamano ni haki ya kimsingi ya raia lakini kinachotokea kwa sasa ni baadhi ya wanasiasa kufanya maandamano kama ndiyo ofisi zao za kazi huku jamii nyingine ikiathiriwa kiuchumi kitu ambacho kinasababisha kwa njia moja au nyingine, kuwepo na anguko la kiuchumi.

Kuna umuhimu ukubwa yakaangaliwa kwa faida ya taifa kwa ujumla.
 

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
sijamuelewa huyu mbunge anayesema eti kuwadhihaki. labda aje na tafsiri halisi ya neno kudhihaki. huenda kwake ikaonekana ni dhihaka kumbe wengine wako serious. kuwa viongozi hakuwafanyi wawe tofauti na binadamu wengine labda kama hawakuwa binadamu na walikuwa hata chooni hawaendi,

Hoja ya Lema ya kupinga mswada wa kuzuia maandamani ni nzuri. kwa mara ya kwanza nasema namuunga mkono huyu jamaa, lakini hata hivyo sitamsogelea maana naweza pigwa tofali. chezea lema wewe, nikifikiria ya mwigamba, ashukuru mungu halikumpata.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom