Mbunge wa CCM mbaroni

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Friday, 07 October 2011 19:43
Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Mbarali (CCM), Modestus Kilufi amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumtishia maisha mtendaji wa kata moja katika jimbo lake.Akizungumza kwa simu jana akiwa chini ya ulinzi wa polisi, mbunge huyo alisema alikamatwa akiwa jimboni kwake Mbarali na kusafirishwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi Mbeya Mjini.

“Nimekamatwa na polisi. Wamekuja polisi wengi wakiwa na silaha na gari. Nilikuwa Mbarali na sasa wananipeleka Mbeya Mjini,” alisema Kilufi na kuongeza:

“Nimewauliza tatizo ni nini wakasema eti nimemtishia Ofisa Mtendaji wa Kata na nilipowauliza kwa nini hawakunipigia simu kwamba nahitajika kituoni hawakutaka kunisikiliza,” alisema.

Alisema anashangaa polisi hao kutompigia simu na kumweleza kuwa anatafutwa ili afike mwenyewe kwa kuwa yeye ni kiongozi na badala yake kwenda kumkamata Mbarali ili wampeleke Mbeya Mjini.

“Hayo ndiyo yamenikuta. Huyo mtu wanayesema nimemtishia maisha sijawahi hata kukutana naye tangu nimetoka bungeni, kwa sasa tupo maeneo ya Uyole ndiyo tunaelekea Mbeya Mjini, wako askari kama wanne, watano hivi, ngoja tukasikie kitakachotokea huko,” alisema mbunge huyo jana saa 11.45 jioni kupitia simu yake ya mkononi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Anaclet Malindisa alithibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo. Hata hivyo, alisema ni mapema kueleza sababu za kukamatwa kwake hadi hapo mawasiliano yatakapofanyika.

 

mwacheni77

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
763
209
Jeshi la police si lina kampeni ya UTII WA SHERIA BILA KUSURUTISHWA inakuaje wanamkamata mbunge kama jambazi,ila jamaa fikira zake police wapo kwa ajiri ya upinzani atiwe abadu kidogo
 

undugukazi

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
315
82
Sasa mmeamini tanzania kuna serikali isiyoangalia vyama kila raia ana haki ya kushtakiwa bila kujali chama...big up sana kwa hili
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,866
986
Nadhani huyo atakuwa na beef na RPC au ukifuatilia vizuri kuna mkono wa mtu mkubwa wananyang'anyana wanawake. Ebu ngoja tuje tusikie stori kamili kama hawakuamua kuyamaliza kimya kimya nje ya vyombo vya habari.
Tafadhali wenzetu wa media msiache kutuletea stori hii hadi mwisho wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom