Mbunge wa Bunda Vijijini stuka, muda umeisha

mbuyamore

Member
Joined
Oct 25, 2018
Posts
37
Reaction score
20
Serikali iligawa wilaya ya bunda na kuongezeka majimbo mawili ambayo ni Bunda vijijini na Bunda mji. Awali ilikuwa jimbo la Bunda ambalo mbunge alikuwa ndg Wassira na Mwibara mh Lugora ambaye ni mbunge hadi sasa.

Tangu achaguliwe huyu mbunge wa Bunda vijijini hajawahi kuzungukia jimbo kujua walau kero na changamoto za wanajimbo tofauti na wabunge wenzake. Cha kushangaza hata bungeni hatujawahi kumsikia akitoa hoja wala kuuliza swali kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake.

Ingawa asilimia kubwa ya wananchi wa Bunda vijijini ni wakulima wa pamba na baadhi ni wafugaji wakubwa lakini umaskini umekithiri jimbo hili kwa sababu ya Sera, mipango mibovu ya halmashauri.

Barabara mbaya hazipitiki wakati wa mvua, maji ni shida hata visima hakuna. Vile vile bei kwa zao la pamba ( ambayo ni kama dhahabu hapa wilayani) ni changamoto tofauti na mazao mengine ya biashara kwa wenzetu mfano korosho Mtwara, Kahawa Bukoba na Moshi.

Mbunge wetu wala hashughuliki na hizi changamoto. Sisi wananchi tunamsubiri kwenye uchaguzi kama atarudi maana hatuna namna kwa sasa ya kumwajibisha katiba yetu imetunyima fursa ya kuwaajibisha viongozi wa aina hii ya mbunge wetu.
 
Sijawahi kusikia mbunge akijipatia yeye mwenyewe budget ya ujenzi wa mabarabara na mengine mwenye ilo jukumu ni serikali kuu huu ujumbe tafadhali naomba uufowadi kwa mh kingstone from Jamica
 
Wewe unaita kweli..
Kwani kuna Jimbo la Bunda vijijini, kwani kuna Mbunge!?
Sijawahi kumsikia, sijui jina lake
 
Ninyi watu wa Bunda nawashauri mumrudishe Mhe. Wassira Bungeni. Mhe. Wassira amefanya mengi sana alipokuwa Mbunge wa Bunda. Mabwawa yote, Shule za Sekondari, TASAF na mengine mengi yametokana na Mhe. Wassira. Mimi namkubali sana Mhe. Wassira ni mfuatiliaji na hakuna kijiji ambacho Mhe. Wassira hakufika.
 
Yupo mkuu, huwezi kumsikia ndo maana ya hiyo post. Bunda vijijini yupo mwanaume.
 
Sijawahi kumsikia sehemu yoyote. Na wala simjui jina. Kumbe yupo na kuna jimbo linaitwa Bunda (V)? Kwa kweli amejituliza kwake kama kasuku.
 
Wakati unatoka nyumbani umehakikisha kuwa umeiachia familia yako kodi ya meza inayowatosha kisawa sawa au ndo umekurupuka kununua bando na kuja jf ili upost!

Alafu sijawahi kusikia mbunge akijipatia yeye mwenyewe budget ya ujenzi wa mabarabara na mengine mwenye ilo jukumu ni serikali kuu huu ujumbe tafadhali naomba uufowadi kwa mh kingstone from Jamica
Hebu tusaidie, unafikiri kazi ya mbunge ni nini labda ?
 
Amekesha, amehonga, ameroga ili tu mumpe uwakilishi, alafu ninyi mnaamini kweli amefanya hayo yote ili awatumikie?
 
Huyo mpumbavu aliwahi kunichukulia demu wangu bwege huyo,yaani nilipopata taarifa kawa mbunge nilisikitika sana,ila nilichomfanya hata kaa asahau bwege huyo,nashukuru MUNGU huyo demu aliachana naye nami pia nkampiga chini
 
Serikali iligawa wilaya ya bunda na kuongezeka majimbo mawili ambayo ni Bunda vijijini na Bunda mji. Awali ilikuwa jimbo la Bunda ambalo mbunge alikuwa ndg Wassira na Mwibara mh Lugora ambaye ni mbunge hadi sasa.

Tangu achaguliwe huyu mbunge wa Bunda vijijini hajawahi kuzungukia jimbo kujua walau kero na changamoto za wanajimbo tofauti na wabunge wenzake. Cha kushangaza hata bungeni hatujawahi kumsikia akitoa hoja wala kuuliza swali kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake.

Ingawa asilimia kubwa ya wananchi wa Bunda vijijini ni wakulima wa pamba na baadhi ni wafugaji wakubwa lakini umaskini umekithiri jimbo hili kwa sababu ya Sera, mipango mibovu ya halmashauri.

Barabara mbaya hazipitiki wakati wa mvua, maji ni shida hata visima hakuna. Vile vile bei kwa zao la pamba ( ambayo ni kama dhahabu hapa wilayani) ni changamoto tofauti na mazao mengine ya biashara kwa wenzetu mfano korosho Mtwara, Kahawa Bukoba na Moshi.

Mbunge wetu wala hashughuliki na hizi changamoto. Sisi wananchi tunamsubiri kwenye uchaguzi kama atarudi maana hatuna namna kwa sasa ya kumwajibisha katiba yetu imetunyima fursa ya kuwaajibisha viongozi wa aina hii ya mbunge wetu.
Mtoeni anaonekana ni mjinga huyo. Ni wa chama gani?
 
Sijawahi kusikia mbunge akijipatia yeye mwenyewe budget ya ujenzi wa mabarabara na mengine mwenye ilo jukumu ni serikali kuu huu ujumbe tafadhali naomba uufowadi kwa mh kingstone from Jamica
Anaowajibu wa kuihabarisha serikali hali halisi na changamoto za watu wake.

Kutokuwa na mfuko sio kigezo cha kuanza vikao bungeni mpaka bunge linaisha uko kimya utadhani wananchi wake hawana shida.

Msiweke wawakilishi kimazoea wananchi wajifunze kuachana na wanaonunuliwa na serikali ili wasiwatetee wananchi wao.

Mleta mada nenda ukaeneze ushauri mzuri utakaoona unafaa kwa watu wote huko ili wasifanye kosa kumchagua mwenye kupuuuza kero zenu.
Kuna wabunge wajinga sana
 
Musimulaumu mbunge wenu amezidiwa na kazi nzito ya kuunga mkono juhudi za muheshimiwa,kazi ya kusema ndiyoooo mbungeni siyo mchezo.
 
Ninyi watu wa Bunda nawashauri mumrudishe Mhe. Wassira Bungeni. Mhe. Wassira amefanya mengi sana alipokuwa Mbunge wa Bunda. Mabwawa yote, Shule za Sekondari, TASAF na mengine mengi yametokana na Mhe. Wassira. Mimi namkubali sana Mhe. Wassira ni mfuatiliaji na hakuna kijiji ambacho Mhe. Wassira hakufika.
Kama unampenda Sana kamchukue ukalale naye akupige miti usiku kucha!
 
Zile T- Shirts na Kanga za Kijani mliozopewa wakati wa Kampeni ndiyo Madhala yake hayo...Vumilieni tu.
 
Type full movie basi.

Back
Top Bottom