Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni!
Hawa jaamaa wa magamba mbona hawaeleweki!!??
Huyu kaomba ruhusa bungeni anaenda msibani kumbe anaenda kwenye 'kujisafisha'.
Na sio ajabu juzi juzi mwingine kaomba ruhusa kumpeleka mama yake India kwa matibabu kumbe anaenda Italy/Uturuki kwenye 'shughuli' zake!
Badwel afiwa, kesi yake yahairishwa
Mwananchi: Monday, 06 August 2012 22:07 Tausi Ally
KESI ya tuhuma za rushwa, inayomkabili Mbunge wa Bahi, Omary Badwel (CCM) imeshindwa kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu mshtakiwa huyo amefiwa na dada yake. Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Lizzy Kiwia alidai kwa Hakimu Mkazi Faisal Kahamba kuwa, kesi ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
"Tuna shahidi mmoja lakini mshtakiwa amefiwa na dada yake," alidai Kiwia. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Kahamba aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.
Badwel katika kesi hiyo namba 146 ya mwaka 2012, anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa na anatetewa na Wakili Mpale Mpoki.
Katika hatua hiyo ya awali, mshtakiwa alisomewa maelezo ya mashtaka na kupewa nafasi ya kubainisha mambo au maelezo anayoyakubali na asiyoyakubali, ambayo upande wa mashtaka utapaswa kuleta ushahidi mahakamani kuyathibitisha.
Badwel anadaiwa kunaswa na Takukuru akipokea rushwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Sipora Liana katika Hotel ya Peacock Dar es Salaam, baada ya kumwekea mtego.
Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 4, 2012 na alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Janeth Machullya akisaidiana na Ben Lincolin, lakini mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo.
Katika shtaka la kwanza, Machullya alidai kwamba mshtakiwa huyo aliomba rushwa ya Sh8 miloni kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Machullya alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Mei 30 na Juni 2, mwaka huu maeneo tofauti Dar es Salaam.
Katika shtaka la pili, Machullya alidai kuwa mshtakiwa huyo alikamatwa Juni 2, Hoteli ya Peacock Dar es Salaam akipokea rushwa ya Sh1 milioni, kutoka kwa Liana.
Alidai kuwa mshtakiwa huyo akiwa Mbunge wa Bahi na mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), aliomba kiasi hicho cha fedha ili kuwashawishi wajumbe wa kamati hiyo wapitishe taarifa yake ya fedha ya mwaka 2011/12.
Machullya alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa yote hayo kinyume cha kifungu cha 15(1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, namba 11 ya mwaka 2007.
Alifafanua kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru, mbunge huyo ni mtumishi wa umma na kitendo hicho ni kinyume cha kanuni zake za kazi.