Mbunge wa Bahi -Omar Badwel asema kesi yake ina mkono wa Takukuru na Wanasiasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa Bahi -Omar Badwel asema kesi yake ina mkono wa Takukuru na Wanasiasa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Aug 7, 2012.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa jimbo la Bahi Omar Badwel amesema kesi yake ya rushwa inayo mkabiri imetengenezwa kwa lengo la kumuua kisiasa,amesema njama hizo zimepangwa na wanasiasa na Takukuru Makao makuuu,alisema kama kweli angekua amekula rushwa Chama chake CCM kingechukua hatua kali juu yake lakini kwa kuwa hata CCM imegundua ni uzushi ndio maana yupo salama na anaendelea kuwa Mbunge,"wananchi msiwe na wasiwasi mimi ni mbunge wenu na nitaendelea kuwa Mbunge wenu haya mnayo yaona ni uzushi tu wa wanasiasa na hao wanao jiita Takukuru" kauli hizo alizitoa katika kijiji cha Chibelela na Mwitikila Jimboni Bahi Mkoani Dodoma,akiwa Mwitikila alito laki 5 kwa kikundi cha washonaji nguo na kuwambia kuwa waendelee kumuombea ashinde kesi yake na wafitini wote waumbuke!
   
 2. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Maji yamemfika....mkumbusheni asiongee mambo yaliyo mahakamani! Makinda alishatuonya
   
 3. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  hiyo laki 5, aliyotoa nayo ichunguzwe ,pengine ni sehemu ya fedha chafu alizopokea rushwa!
   
 4. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Wizi mtupu anatafuta huruma kwa wananchi hamna lolote
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mwizi amekamatwa na taasisi iliyotungwa na bunge, iko kisheria na inatumia kodi zetu pamoja na mambo mengine! haikuwa na haja kuendelea kutumia fedha ya walipa kodi kwenda mahakamani! alitakiwa apigwe mvua tano na ubunge umchomoke!
   
 6. Y

  Yetuwote Senior Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana CCM haijampa adhabu kwa ufisadi na rushwa kwa kuwa ni sera yao.
   
 7. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,996
  Likes Received: 6,778
  Trophy Points: 280
  Huyo jamaa anasema hajapokea rushwa ndiyo maana chama chake hakijamchukulia hatua, hivi ni lini chama cha magamba kimewachukulia hatua wala rushwa wake? Hivi tujiulize kampeni yao ya kuvuana magamba, mbona imekufa kifo cha mende!! Hebu tujiulize kila mtu anajua Chenge amelamba rushwa ya rada, lakini mbona hawamchukulii hatua, wanajua kuwa kama watamchukulia hatua, atatumia staili ya wao wamemwaga ugali wacha na mm nimwage mboga!! Wataumbuka wengi, hata yule jamaa dhaifu wa magogoni hatapona!!
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  eti kesi yake ina mkono wa TAKUKURU hajui kua kazi ya TAKUKURU ni kuwakamata watu ka nyie..na yeye awe ndio mfano wa kuigwa...bado wako wabunge wengi tu dodoma pale wala rushwa..ukigundulika umekula rushwa unapigwa chini ubunge hamna mjadala hapo
   
 9. B

  Bob G JF Bronze Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm nani hapokei rushwa na hatoi rushwa? ccm ndo mama wa rushwa na ndio maana haichukui hatua kwa wabunge wake wanaotoa na kupokea rushwa, na Utetezi wake ni wakitoto mno
   
 10. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni!
   
 11. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,322
  Likes Received: 2,687
  Trophy Points: 280
  Hao anao walaumu alikuwanao wakati anapokea rushwa?.anataka ccm waseme nini wakati wao ndio waasisi wa warushwa na kwao rushwa siyo haramu na kwamba ndio silaha yao kuu ya kujipatia ushindi.(ccm bila rushwa ushindi haupo).
   
 12. a

  anney Senior Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Badwell inasemekana alitokwa na haja ndogo alipoambiwa yupo chini ulinzi.Nafikiri amejisahau sasa. Anaongea kwa kiburi maana atakuwa ameshahonga huko mahakamani. CCM kazi yake nikulea wala rushwa mbona watanzania wanalifahamu hilo!
   
 13. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naungana na hoja ya Kafulila aliyo sema Mbunge wa Bahi asimamiswe ubunge hadi kesi yake itakapo isha,sasa kwa uzembe huu wa kanuni za bunge na hata udhaifu taratibu za kinidhamu za bunge na CCM ina mpa uhalali wa mwizi kutamba mitaani na kuingia bungeni na kua na jeuri ya kujiona hakuna anae weza kumsumbua!
   
 14. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh. Baduel acha kuwadanganya wananchi, halafu inaonesha ni kwa kiasi gani hujui sheria, unaharibu kesi yako mwenyewe kwa kuitolea uamzi nje ya mahakama! sasa subiri kichapo mahakamani!
   
 15. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Hawa jaamaa wa magamba mbona hawaeleweki!!??
  Huyu kaomba ruhusa bungeni anaenda msibani kumbe anaenda kwenye 'kujisafisha'.
  Na sio ajabu juzi juzi mwingine kaomba ruhusa kumpeleka mama yake India kwa matibabu kumbe anaenda Italy/Uturuki kwenye 'shughuli' zake!

  Badwel afiwa, kesi yake yahairishwa
  Mwananchi: Monday, 06 August 2012 22:07 Tausi Ally

  KESI ya tuhuma za rushwa, inayomkabili Mbunge wa Bahi, Omary Badwel (CCM) imeshindwa kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu mshtakiwa huyo amefiwa na dada yake. Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Lizzy Kiwia alidai kwa Hakimu Mkazi Faisal Kahamba kuwa, kesi ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

  "Tuna shahidi mmoja lakini mshtakiwa amefiwa na dada yake," alidai Kiwia. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Kahamba aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.

  Badwel katika kesi hiyo namba 146 ya mwaka 2012, anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa na anatetewa na Wakili Mpale Mpoki.

  Katika hatua hiyo ya awali, mshtakiwa alisomewa maelezo ya mashtaka na kupewa nafasi ya kubainisha mambo au maelezo anayoyakubali na asiyoyakubali, ambayo upande wa mashtaka utapaswa kuleta ushahidi mahakamani kuyathibitisha.

  Badwel anadaiwa kunaswa na Takukuru akipokea rushwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Sipora Liana katika Hotel ya Peacock Dar es Salaam, baada ya kumwekea mtego.
  Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 4, 2012 na alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Janeth Machullya akisaidiana na Ben Lincolin, lakini mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo.

  Katika shtaka la kwanza, Machullya alidai kwamba mshtakiwa huyo aliomba rushwa ya Sh8 miloni kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.

  Machullya alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Mei 30 na Juni 2, mwaka huu maeneo tofauti Dar es Salaam.

  Katika shtaka la pili, Machullya alidai kuwa mshtakiwa huyo alikamatwa Juni 2, Hoteli ya Peacock Dar es Salaam akipokea rushwa ya Sh1 milioni, kutoka kwa Liana.

  Alidai kuwa mshtakiwa huyo akiwa Mbunge wa Bahi na mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), aliomba kiasi hicho cha fedha ili kuwashawishi wajumbe wa kamati hiyo wapitishe taarifa yake ya fedha ya mwaka 2011/12.

  Machullya alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa yote hayo kinyume cha kifungu cha 15(1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, namba 11 ya mwaka 2007.

  Alifafanua kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru, mbunge huyo ni mtumishi wa umma na kitendo hicho ni kinyume cha kanuni zake za kazi.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwanini anaongelea jambo LILILO MAHAKAMAN?????
   
 17. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naunga Mkono. Ni kweli kaonewa. Mbona hako ka mtindo ka Takrima wote wanakatumia?? Iweje leo yeye tu ndiyo kasheria haka kamfike????? Tuna mifano mingi, ya wengi waliochukua takrima, na hao wanao jiita taasisi hawafanyi kazi, iweje leo kachukua tuvijisenti, wanakuja juu???????? Huo ni uonevu.
   
 18. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,971
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hebu nikumbusheni ni lini? Ccm imesheghulikia wala rushwa?
   
 19. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh kweli wanajuana yaleyale ya mhando wa tanesco kaftiniwa kwa kuinyima puma isiyo na uwezo tenda
   
 20. k

  kally the great Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  badwel anaonewa. tunafahamu msimamo wake kuhusu uchimbaji wa urani unaotarajiwa kufanyika jimboni kwake hivyo aliwaandaa wananchi wake wasihame bila malipo sasa hiyo imewakera wakubwa ndo maana wanataka wamuondoe ubunge! ninavyomfahamu anamiliki vituo viwili vya mafuta na alikuwa na pesa kabla hajawa mbunge. huo ndo ukweli
   
Loading...