Mbunge Salum Khamis Salum 'Mbuzi' (CCM) apewa mgodi hifadhini!

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
MMOJA kati ya wabunge ndani ya Bunge la 11 yupo katika mtihani mzito akishutumiwa kushiriki katika kujipatia eneo la uchimbaji wa madini ndani ya eneo la hifadhi ya wanyamapori bila ridhaa ya wadau wakiwamo wanakijiji.

Taarifa zilizolifikia Raia Tanzania zinadai kwamba, Mbunge wa Meatu, Salum Khamis Salum ‘Mbuzi’ (CCM) alitumia ushawishi alionao kisiasa na kufanikisha upatikanaji wa leseni ya kuchimba shaba katika eneo la Gururum, Meatu mkoani Simiyu.

Mbuzi alifanikiwa kurejea tena bungeni baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana kwa kulipa kisasi na kumwangusha mpinzani wake wa mwaka 2010, Meshack Opurukwa (Chadema), aliyedumu bungeni kwa msimu mmoja tu.

Mbuzi pamoja na washirika wake, Enock Yakobo na Abdillahi Lessani walipewa leseni hiyo Novemba 18, 2014.

Leseni hiyo ilisainiwa na Ofisa Madini Kanda ya Ziwa, Mhandisi Juma Semanta, na itadumu kwa miaka saba.

Hata hivyo, upatikanaji wa leseni huo haujawaridhisha wadau kadhaa wa ardhi na mazingira kwani mbali na sheria kuzuia uchimbaji madini ndani ya eneo hilo, wadau wengine muhimu pia hawakuhusihwa katika upatikanaji wake.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao jirani na lilipo eneo hilo Anthony Philipo, ameliambia Raia Tanzania kwamba hajawahi kushirikishwa wala kujulishwa kuhusiana na utolewaji wa leseni ya uchimbaji wa madini katika hifadhi ya Mwiba, eneo ambalo kijiji hicho kilikodisha kwa wawekezaji wa Kimarekani mwaka 2008.

Anthony ambaye pia ni Diwani wa Makao alisema hana taarifa zozote kuhusu mgodi wa shaba na kuongeza, "sina taarifa zozote kuhusu mgodi huo na sijawahi kuona watu wa mazingira na hatujui nani mmiliki."

Baadhi ya watendaji wa wilaya ya Meatu wameelezwa kulalamikia hatua hiyo lakini wamekua wakimuogopa Mbunge huyo ambaye wamesema ana nguvu kubwa na ushawishi.

“Kwa kifupi ni kwamba kuna namna ilifanyika ili watu hawa pamoja na Mbunge wetu wa sasa wapatiwe leseni hiyo. Sisi wananchi na hata viongozi wa kijiji hatufahamu lolote na wala hatukuhusika,” alisema mwanakiji ambaye hakutaka kutajwa jina.

Upatikanaji huo wa leseni ni kinyume cha sheria za nchi zinazoelekeza kuwapo kwa ushirikishwaji wa pande kadha wa kadha zinazohusika.

Eneo kubwa la Meatu ni la hifadhi ingawa ukweli ni kwamba limevamiwa na wafugaji wa ndani na nje ya nchi na kuwapa wakati mgumu watunzaji na wahifadhi wa mazingira kama vile.

Raia Tanzania lilimtafuta Mbuzi kwa njia ya simu jana, lakini hakupokea simu yake ya mkononi, na baada ya kuandikiwa ujumbe mfupi wa maandishi, aliujibu kwa kuahidi kuzungumza na mwandishi wetu, ahadi ambayo hakuitekeleza hadi tulipokuwa tunakwenda mitamboni.

Source Raia Tanzania Leo Ijumaa, Aprili, 15, 2016
1460692170173.jpg


================

Update;

Mbunge apigwa "stop"

*Mpango wake wa kuchimba madini hifadhini wakwama

*Kijiji chatangaza mgogoro na mwekezaji RC aahidi kuutatua

NA MWANDISHI WETU, Meatu

SERIKALI mkoani Simiyu imesitisha mpango wa Mbunge wa Meatu, Salum Salum ‘Mbuzi’ kutaka kuchimba madini ndani ya pori la hifadhi ya wanyamapori linaloendeshwa kisheria na kampuni ya Mwiba Holdings Limited.

Zuio hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ikiwa ni siku chache baada ya kubainika kwamba Mbunge huyo amepewa kibali kuanzisha uchimbaji shaba katika eneo la Gururum ndani ya pori hilo.

Wiki iliyopita, Raia Tanzania liliripoti shutuma dhidi ya Mbuzi, aliyedaiwa kutumia ushawishi alionao kisiasa na kufanikisha upatikanaji wa leseni ya kuchimba madini katika eneo hilo lililomo ndani ya Hifadhi ya Mwiba, Meatu mkoani Simiyu.

Mbuzi akiwa na washirika wake kibiashara, Enock Yakobo na Abdillahi Lessani, walipewa leseni hiyo Novemba 18, 2014, ikiwa imesainiwa na Ofisa Madini Kanda ya Ziwa, Mhandisi Juma Semanta, yenye uhai wa miaka saba ingawa upatikanaji wake haukuwaridhisha wadau kadhaa wa ardhi na mazingira kwani haukuzingatia sheria na taratibu husika.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa wakazi wa kijiji cha Makao mwishoni mwa wiki, Mtaka aliwataka wanasheria na maofisa madini wa Simiyu kusitisha mpango huo ili kuepusha migogoro zaidi ya kimaslahi katika eneo hilo.

“Tunasitisha huo mpango kazi wa kuchimba madini. Kinachowagombanisha hapa ni uamuzi ambao ninyi mliufanya huko nyuma, leo mnasema hamna eneo la kuchunga mifugo. Kwa hiyo habari ya madini hapana,” alisisitiza mkuu huyo wa mkoa.

Mbunge wa Meatu, Salum Mbuzi, hakupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo.

Katika hatua nyingine, Mtaka alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu, Godfrey Machumu, kuhakikisha Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Makao, Isack Magaka, anakamatwa kwa kosa la kutohudhuria mkutano huo ulioitishwa maalumu kujadili mgogoro uliopo.

Kabla ya hapo, Mtaka alimwita Magaka awaeleze wanakijiji taarifa ya mapato na matumizi ya fedha zinazotolewa na Kampuni ya Mwiba, lakini ikabainika kwamba hakuwepo mkutanoni hapo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao, Anthony Philip, alikiri kwenye mkutano huo kwamba kijiji hicho kimekuwa kikipokea Sh. milioni 115 zikiwamo Sh. milioni 80 za kodi ya pango kila mwaka kutoka Kampuni ya Mwiba yenye mkataba wa kuendesha shughuli za uwindaji wa kitalii na upigaji picha katika pori hilo.

Mbali ya kiasi hicho cha fedha, Meneja Uhusiano wa Mwiba Holdings Limited, Clarence Msafiri, alisema kampuni hiyo pia imekuwa ikikipatia kijiji shilingi milioni mbili kila mwaka kama kodi ya uwanja wa ndege na fedha nyingine nje ya makubaliano yao kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa miradi ya kijamii kijijini hapo.

“Mfano sasa hivi tumejipanga kuchangia ununuzi wa madawati kwa ajili ya wanafunzi shuleni kuitikia wito wa Rais John Magufuli,” alisema Msafiri.

Kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Kijiji cha Makao na kampuni ya Mwiba, Mkuu wa Mkoa, Mtaka, alimtaka Mwenyekiti wa Kijiji kwa niaba ya wanakijiji kutangaza kusudio la mgogoro na kampuni hiyo ili liwekwe kwenye maandishi na hatimaye Serikali ilitafutie usuluhishi wa kisheria.

“Kamati ya Ulinzi na Usalama (ya mkoa) imesikiliza (tuhuma dhidi ya Mwiba). Kwa kuwa jambo hili ni la kisheria, sheria inamtaka Mwenyekiti wa kijiji atangaze kusudio la mgogoro na Kampuni ya Mwiba kisha tutafute usuluhishi kukiepushia kijiji hiki matatizo,” alisema Mtaka.

Baadaye Mwenyekiti wa kijiji, Philip, alipewa nafasi na kusema: “Ninatangaza kusudio la mgogoro na Kampuni ya Mwiba.”

Mgogoro huo unadaiwa kuikwamisha Kampuni ya Mwiba kukabidhi Sh. milioni 356 ilizotenga mwaka huu kwa ajili ya kuchangia gharama za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika vijiji vya Makao, Iramba Ndogo, Mwangudo, Sapa, Mbushi, Jinamo na Mwabagimu vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) katika eneo hilo.

Kumekuwepo na tuhuma zinazoelekezwa kwa Philip, kwamba ndiye chimbuko la mgogoro huo pamoja na baadhi ya wanakijiji wakidai kuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Mwiba wamekuwa wakiwanyanyasa watu wanaokutwa wakichunga mifugo ndani ya pori hilo. Hata hivyo, mwenyekiti huyo alipoulizwa alikana tuhuma hizo.

 
wanataka kuwa viongozi kwa gharama yoyoye ile ili kuiba na kutolipa kodi kwa mgongo wa ubunge huku wachimba chumvi wakikamuliwa...
 
Mbunge (Mbuzi) ni mchimbaji wa madini na tayari amekwisha pata leseni ya kuchimba madini aina ya copper ndani ya WMA ya Makao eneo ambalo mwekezaji mwingine MWIBA Holdings alishapewa awali kwa shughuli za uhifadhi na uwindaji. Mbunge anaelewa vizuri uchimbaji wa madini na uhifadhi ni shughuli ambazo hazilandani au itambidi kuingia gharama kubwa sana ili aweze kuendeleza uchimbaji wa madini katika eneo hilo alilolipata bila kufuata taratibu na ameanza kusema uongo kila mahali kuchafua jina la mwekezaji MWIBA Holdings anyanganywe vibali na yeye (Mbuzi) kuingia mkataba wa uchimbaji wa madini na vijiji vya eneo hilo.

Mwanzoni mwa mwezi Machi mbunge huyu aliongea kwa uchungu sana mbele ya waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akilalamika kuhusu mwekezaji MWIBA Holdings aliyepewa eneo la kijiji kwa mikataba halali kuwekeza kwenye shughuli za utalii na pia kutunza mazingira ya eneo husika. Alimtuhumu mwekezaji huyo tena bila kumungunya maneno kwamba hana mikataba halali na kwamba ile iliyopo imepatikana kwa njia za udanganyifu. Jambo ambalo si kweli, inajulikana wazi vibali hivyo vilipatikana kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa na sheria ya nchi hii na serikali ya kijiji ikihusishwa tangu mwanzo.

Mbunge huyu ni mwananchi wa eneo hilo alikuwa wapi miaka yote hiyo akashwindwa kulalamika au kuhakikisha mwekezaji wa MWIBA Holdings anachukuliwa hatua stahiki (kwa sababu ni mtu mwenye nafasi katika jamii) akangoja mpaka alipopata Primary Mining Licence November 2014? Kibali kinachomruhusu kuchimba copper eneo ambalo mwekezaji mwignine alishafanya mkataba wa halali na vijiji husika? Kama lengo lake ni kutetea haki za wananchi wa Meatu angejitokeza tangu mwanzo kumu expose mwekezaji huyu?

Mbunge (Mbuzi) badala ya kutambua kazi kubwa inayofanywa na mwekezaji MWIBA Holdings kwenye jamii iliyotoa ardhi yake kwa hiari kwa ajili ya uhifadhi na utalii anaeneza uongo kuchafua jina mwekezaji huku akimdanganya Waziri Mkuu. Hivi majuzi Mbunge huyo pamoja na Diwani wa eneo hilo (ambae pia ni mwenyekiti wa kijiji cha Makao) katika kikao cha changizo la wadau kwa shughuli za maendeleo Mbunge huyo bila aibu aliwazuia kampuni yaMWIBA Holdings kutoa mchango wa TZS 356,280,900 kwa shughuli za maendeleo akidai kuna mgogoro jambo embalo sio kweli. Ikumbukwe pia Mbunge huyu huyu amehusishwa na matukio ya ujangili ikiwa ni pamoja na gari zake kukamatwa katika shughuli za ujangili na kupatina na meno ya tembo.

Huku akijua kuwa wananchi anao wawakilisha ni masikini amekuwa akiwapa fedha na kuwanywesha pombe ili kuonge maneno ya hovyo na kuwatumia wafugaji wanaolitaka eneo hilo kwaajili ya kuchungia kuichafua kampuni ya MWIBA Holdings. Katika kijiji cha Makao na Mwangudo imefanyika jitihada kubwa ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya siri na mikutano ya sungusungu kuwadhibiti vijana ambao wamekuwa tayari kusema ukweli na kukemea ubinafsi unaofanywa na Mbunge huyu na vibaraka wake. Mwenyekiti wa Kijiji hicho na ambaye pia ni diwani amewaagiza na kuwadhibiti wananchi katika mkutano ulioandaliwa kufanyika leo Makao na Mwangudo ili wasiweze kusema chochote huku akiwaandaa vijana maalumu watano tu watakao uliza maswali ambayo yeye anayapenda. Njama hizo za kifisadi zinafanyika kwa ushirikiano wa Mwandishi wa habari wa ITV Bwana Beresi China ambaye amenunuliwa na Mbunge huyo.

Hii ndio aina ya viongozi tuliowachagua kutuwakilisha. Wat ambao wako tayari kufanya lolote kwa manufaa binafsi.
 
katika chaguzi zote za taifa hili ni kipindi ambacho wabunge wa ccm hutumia gharama kubwa sana na hiyo yote hutokana na kiburi kwamba akishinda ubunge basi kila kitu atafanya kwa mgongo wa ccm
 
Ndiyo tulimuona akitokwa jasho TV juu ya uwekezaji wa Mwiba Holdings kumbe ana maslahi ya kwake.Magufuli chukuachama itakwisha.Hata na wabunge nao!!!!!!!
 
Mpaka 2020 kuna dalili kuwa xaidi ya 50% ya wa bunge wa ccm watakua kwenye scandal mbalimbali maana sasa hivi ni kama wanashindana kuhujumu, kula rushwa na dhuluma au udanganyifu
 
Na sisi wananchi tu wajinga sana wakati mwingine. Tunakubali kutumika kishenzi shenzi tukidhani tunajipunguzia njaa kumbe tunajichoma wenyewe.
 
Shaba yenyewe imeporomoka thamani kwenye soko la dunia atapata hasara tu, bora afuate taratibu kwanza huku akisubiria shaba ipande thamani
 
Hhahahahahha

CCM wame make headline tena? daaaaaah

CCM ni wezi sana wa nchi hii

alafu yalivyo majinga yatakuja na porojo za kipuuzi oooh lowasa ooooh sijui nani......sheny type
 
50% ni ndogo sana, JPM mwenyewe na kufurukuta kote yeye pia ana yake.
Mpaka 2020 kuna dalili kuwa xaidi ya 50% ya wa bunge wa ccm watakua kwenye scandal mbalimbali maana sasa hivi ni kama wanashindana kuhujumu, kula rushwa na dhuluma au udanganyifu
 
Ccm katika ubora wao ccm Na ufisadi ni pipa Na mfuniko sitashangaa mkuu Wa majipu naye akiwa kashfa
 
Yule mwenzake wa kishapu alipewa tender na stamigold kuchimba wakati hata vifaa hana za kufanya kazi.
Nakumbuka enzi za escrow alivyo kuwa akitokwa na povu,kumbe alikuwa na maslai na wizara hiyo..
Bunge limejaa wafanya biashara hawa kweli wanaweza kukemea chochote kwenye sector husika,ingali na wao wamewekeza humo humo.ifikie hatua hawa wafanya biashara wasiwe wawakilishi wetu
 
Jamani jamani jamani tunaelekea wapi Watanzania ? Ee mungu tunusuru na kadhia hizi za wabunge waroho wabinafsi na wasio na hata chembe ya huruma.
 
Back
Top Bottom