Mbunge Nape Nnauye amwita Raila Odinga kibaraka

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,276
fb2d2ea8c737a6be38057bf2642586e6.jpg
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kumtabiria ushindi mgombea wa urais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kusema kuwa atashinda uchaguzi huo ambao utafanyika Alhamisi Oktoba 26, 2017 na kusema Uhuru ndiye anayestahili kuongoza nchi hiyo.

Nape Nnauye amedai kuwa Uhuru Kenyatta anastahili kuwa Rais wa Kenya kwa sababu yeye ni mwana demokrasia wa kweli hivyo anaamini raia wa Kenya watampa kura nyingi za kutosha na kumpuuza mpinzani wake Raila Odinga.

"Unastahili kuwa Rais wa Kenya Mwana demokrasia wa kweli. Naamini ndugu zangu wa Kenya watakuchagua kwa kishindo kesho na kumpuuza kibaraka".

Ameandika Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Nchi ya Kenya kesho inategemewa kufanya uchaguzi wa marudio wa nafasi ya urais kufuatia mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya urais.
 
Nafafananisha uchaguz wa marudio wa kenya na zanzibar

Wamefanana kila kitu.Seif alijitoa Shein akapita

nae odinga kajitoa Uhuru atapeta

Hapa ndo hua naamini kwanini CCM kinaitwa chama cha ukombozi Afrika,hivi vyote huiga ccm
 
Ukombozi tena sio mapinduzi?
 
Mbunge wa Mtama CCM, Nape Nnauye amefunguka na kumtabiria ushindi mgombea wa urais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kusema kuwa atashinda uchaguzi huo ambao utafanyika Alhamisi Oktoba 26, 2017 na kusema Uhuru ndiye anayestahili kuongoza nchi hiyo.

Nape Nnauye amedai kuwa Uhuru Kenyatta anastahili kuwa Rais wa Kenya kwa sababu yeye ni mwana demokrasia wa kweli hivyo anaamini raia wa Kenya watampa kura nyingi za kutosha na kumpuuza mpinzani wake Raila Odinga.

"Unastahili kuwa Rais wa Kenya Mwana demokrasia wa kweli. Naamini ndugu zangu wa Kenya watakuchagua kwa kishindo kesho na kumpuuza kibaraka".

Ameandika Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Nchi ya Kenya kesho inategemewa kufanya uchaguzi wa marudio wa nafasi ya urais kufuatia mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya urais.
Wale wapenzi wa magoli ya mkono ni lazima watamuunga mkono Kenyata. Nape usijitoe ufahamu, Kenyata aliiba kura August 8, hilo halina ubishi hata Supreme court iliamua hivyo, sasa unachomsifia Kenyata ni nini? CCM nao ni wezi wa kura ndiyo maana lazima wamsifie mwizi mwenzao.
 
Nape anaweweseka sana!

2005 Wakati akina Nazir Karamagi na Edward Lowassa wanahangaika kusaka Ushindi wa Dkt Kikwete Yeye alikuwa Bize na Sumaye wake kumharibia Jakaya lakin baadae Yeye akala neema za Utawala wa Jakaya na wenzie kina Rostam, Lowassa na Nazir waliompigania wakapigwa chini

2010 Yeye alikuwa bize na Chama chao Mfu cha CCJ Sijui CCk kumsaliti Rais Kikwete

Sasa ni zamu yake Yeye alimpigania Magu sasa kapigwa chini na wanaokula Bata kina Jerry Muro walikuwa Team Lowassa!
Kutesa kwa zamu,Mbona wenzie walivumilia
 
Sasa hapo nape kamtabiria vp uhuru kenyata ushindi wa urais kenya wakati tayari odinga kajitoa ktk uchaguzi huo?!
kilaza wahedi
 
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kumtabiria ushindi mgombea wa urais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kusema kuwa atashinda uchaguzi huo ambao utafanyika Alhamisi Oktoba 26, 2017 na kusema Uhuru ndiye anayestahili kuongoza nchi hiyo.

Nape Nnauye amedai kuwa Uhuru Kenyatta anastahili kuwa Rais wa Kenya kwa sababu yeye ni mwana demokrasia wa kweli hivyo anaamini raia wa Kenya watampa kura nyingi za kutosha na kumpuuza mpinzani wake Raila Odinga.

"Unastahili kuwa Rais wa Kenya Mwana demokrasia wa kweli. Naamini ndugu zangu wa Kenya watakuchagua kwa kishindo kesho na kumpuuza kibaraka".

Ameandika Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Nchi ya Kenya kesho inategemewa kufanya uchaguzi wa marudio wa nafasi ya urais kufuatia mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya urais.

Wewe unamuandikia nape kwani we we pekee huwezi kujiongoza?ni aibu sana Ku coly na Ku paste alichoandika MTU,tumia akili yako na sii kusubiri wenzio wakusaidie
 
Back
Top Bottom