Mbunge Msigwa: Tususie bidhaa za wafanyabiashara wanaounga mkono ukandamizaji Demokrasia

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kupitia akaunti yake ya Twitter akiwataka wale wote wapenda demokrasia na haki za binadamu wasusie bidhaa za wafanyabiashara wanaoenda kinyume na matakwa hayo.

Kwa wale wanaochambua kwa undani ujumbe wa msigwa watakubaliana na mimi kuwa ujumbe wa Msigwa ulikuwa unaelekezwa kwa serikali kwa sababu haya ni madai ya CHADEMA kwa serikali. Kwa maana nyingine, Msigwa alikuwa anawataka wananchi wasusie bidhaa za wafanyabiashara wanaoshirikiana na serikali! Msigwa hajui kuwa hata mshahara na posho anazopokea kama Mbunge ni njia mojawapo inayoonyesha anashirikiana na serikali ya Rais Magufuli kwa sababu zinalipwa na serikali.

Maneno ya Msigwa yananikumbusha maneno ya Kiongozi Mkuu wa Muungano wa National Super Alliance(NASA), Raila Odinga aliyewaasa wafuasi wake wasusie bidhaa za makampuni matatu ambayo ni Safaricom, Brookeside na Bidco kwa sababu yanatoa ushirikiano kwa Rais Kenyata na Jubilee.

Kinachofurahisha zaidi ni kuona kuwa anachokifanya Msigwa ndicho kile ambacho CHADEMA wakiongozwa na Msigwa walimcheka Odinga alipotoa tamko la kususia badhaa za makampuni hayo.

Anachokifanya Msigwa hakina tofauti sana na kile kilitokea kwa Lowassa ambapo wakati akiwa CCM walimuita ni fisadi namba moja na hafai hata kupewa fomu ya kugombea Urais lakini alipoachwa na CCM wakamkimbia na kumfanya Mgombea Urais bila hata uwepo wa mchakato kulingana na Katiba, Taratibu na Kanuni za CHADEMA.

Huu ndio ujumbe wa Mbunge Msigwa.
View attachment 704475
Basi asusie mshahara na marupurupu anayoyapata akiwa kama mbunge,kwani mishahara na marupurupu hayo yanatokana na kodi kutoka viwanda hivyo hivyo anavyotaka visusiwe,ningemuona Msigwa wa maana kama angesusuia kila kitu kinachopitia kwenye mikono ya serikali na sio viwanda tu,je hao wafanyakazi wa hivyo viwanda anavyotaka watu wasusie wataenda kula kwa mkewe
 
Mchungaji Msigwa yuko sahihi kabisa, acha tu kususia bidhaa za hayo makampuni yaliyo ungana na ccm kudhulumu haki za wa tz, bali hata ikibidi kususia sherehe zote za mikusanyiko za kitaifa, naamini kwa Wale wote ambao wanaona jinsi ccm na vikaragosi wao wanavyo fanya matendo ya ajabu ndani ya Taifa hili watamuunga mkono mch Peter Msigwa, nampongeza kwa wazo makini.
 
halafu bado kuna watu wanahoji kwa nini madiwani wa cdm wanahama chama...ukizingatia huyu ni kiongozi mkubwa tu kwenye chama.

Nahisi kama madesa ya mzee slaa ndo yalikuwa yakiwaweka mjini hawa watu.

Mimi sikushangaa kusima ujumbe wa Msigwa.

Mimi ninawashangaa wale wanamshangaa.

Kwa nini umshangae mtu ambaye aliwahi kusema kazi ya wapinzani ni kuwachochea wananchi ili waichukie serikali na hatima yake waiondoe madarakani.
 
Anachokifanya Msigwa hakina tofauti sana na kile kilitokea kwa Lowassa ambapo wakati akiwa CCM walimuita ni fisadi namba moja na hafai hata kupewa fomu ya kugombea Urais lakini alipoachwa na CCM wakamkimbia na kumfanya Mgombea Urais bila hata uwepo wa mchakato kulingana na Katiba, Taratibu na Kanuni za CHADEMA]

Lowassa aliitwa fisadi namba moja, huku CCM wakimkingia kifua na kumfanyia kampeni za ubunge. Mwenyekiti alisema hiyo ni ajali tu ya kisiasa. Unayakumbuka haya?
 
Na wana CCM wasuse kununua nyanya zake?

msigwa-2-jpg.521888
 
Usipuuze theory, maana kuna maeneo huwa inakuwa practical. Hapa nilipo kuna mfanyabiashara mkubwa sana miaka miwili iliyopita watu walianza kama utani vile kususia bidhaa zake kwa sababu za kisiasa,hadi kufikia mwaka jana akawa amefunga duka lake kubwa la jumla na sheli.Hivi sasa ametia akili kichwani,ameacha upumbavu na ushabiki na badala yake anatumia critical thinking ktk maamuzi siyo maswala ya ndiyoooo!
 
HABARI,
"MsemajiUkweli,
Msigwa angetaja hao wafanyabiashara na makampuni yao ila kama kutakuwa na makampuni ya chai nyanya atakuwa amejiangamiza yeye mwenyewe,Sidhani hilo ni suluhisho kwani ni kuongeza umasikini kwa wakulima wakati wao wenyewe wanaposho na mishahara mikubwa na mwisho wa miaka mitano wanapokea posho kubwa na kuwaacha wananchiwake wakiumia kwenye lindi la umasikini.

LUMUMBA
Kwani lini mkulima alipunguziwa umasikini?Kungekuwa na nia ya kuwapunguzia umasikini wasingeweza kujibiwa majibu ya kejeli wakati ule walipokuwa wanalalamika juu ya bei na soko la mbaazi.
 
Afadhari ya huyu ameongea vizuri juu ya hatua za kuchukuwa kwa mtu msiyeendana kimtazamo,kuliko yule anayeteka na kuuwa watu wenye mtazamo tofauti.
 
Usipuuze theory, maana kuna maeneo huwa inakuwa practical. Hapa nilipo kuna mfanyabiashara mkubwa sana miaka miwili iliyopita watu walianza kama utani vile kususia bidhaa zake kwa sababu za kisiasa,hadi kufikia mwaka jana akawa amefunga duka lake kubwa la jumla na sheli.Hivi sasa ametia akili kichwani,ameacha upumbavu na ushabiki na badala yake anatumia critical thinking ktk maamuzi siyo maswala ya ndiyoooo!
Uwongo wa aina hii upeleke facebook.

Hapa kuna motto isemayo, Jamiiforums is where we dare to talk openly.

Sema jina la huyo mfanyabiashara, sehemu aliyokuwa anafanyia biashara(duka la jumla na kituo cha mafuta) na jina la kampuni ili tumjue. Kinyume cha hivyo ni uwongo wa kitoto.
 
Acha uzembe,theory ni nyepesi sana kuihubiri lakini practical inawatia wengi kiwewe.Hapa jamii forum paliwahi kuandikwa kuwa "Baadhi ya mawaziri ni wapumbavu" Nyingine ikaandikwa "Baadhi ya viongozi wa upinzani ni vibaraka wa wazungu" Mbona hukusema watajwe?Ni namna gani inaonyesha unavutwa na upepo badala ya critical thinking.
 
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kupitia akaunti yake ya Twitter akiwataka wale wote wapenda demokrasia na haki za binadamu wasusie bidhaa za wafanyabiashara wanaoenda kinyume na matakwa hayo.

Kwa wale wanaochambua kwa undani ujumbe wa msigwa watakubaliana na mimi kuwa ujumbe wa Msigwa ulikuwa unaelekezwa kwa serikali kwa sababu haya ni madai ya CHADEMA kwa serikali. Kwa maana nyingine, Msigwa alikuwa anawataka wananchi wasusie bidhaa za wafanyabiashara wanaoshirikiana na serikali! Msigwa hajui kuwa hata mshahara na posho anazopokea kama Mbunge ni njia mojawapo inayoonyesha anashirikiana na serikali ya Rais Magufuli kwa sababu zinalipwa na serikali.

Ikumbukwe kuwa Msigwa aliwahi kusema aliwahi kusema kazi ya wapinzani ni kuwachochea wananchi ili waichukie serikali na hatima yake waiondoe madarakani.

Maneno ya Msigwa yananikumbusha maneno ya Kiongozi Mkuu wa Muungano wa National Super Alliance(NASA), Raila Odinga aliyewaasa wafuasi wake wasusie bidhaa za makampuni matatu ambayo ni Safaricom, Brookeside na Bidco kwa sababu yanatoa ushirikiano kwa Rais Kenyata na Jubilee.

Kinachofurahisha zaidi ni kuona kuwa anachokifanya Msigwa ndicho kile ambacho CHADEMA wakiongozwa na Msigwa walimcheka Odinga alipotoa tamko la kususia badhaa za makampuni hayo.

Anachokifanya Msigwa hakina tofauti sana na kile kilitokea kwa Lowassa ambapo wakati akiwa CCM walimuita ni fisadi namba moja na hafai hata kupewa fomu ya kugombea Urais lakini alipoachwa na CCM wakamkimbia na kumfanya Mgombea Urais bila hata uwepo wa mchakato kulingana na Katiba, Taratibu na Kanuni za CHADEMA.

Huu ndio ujumbe wa Mbunge Msigwa.
View attachment 704475
Watu aina ya Msigwa hawapaswi kupewa mwanya ndani ya nchi........sijui uzalendo na uchungaji wao.
 
Tatizo la Msigwa anamuogopa sana Salim Asas kuelekea 2020!
 
Back
Top Bottom