Mbunge Mahawanga Janeth atunukiwa Tuzo ya Heshima na TALGWU

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,922
948
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Mahawanga Janeth amekabidhiwa Tuzo ya Heshima na Wafanyakazi Wanawake wa TALGWU Mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe zilizoandaliwa na Wanawake hao siku ya kilelele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani tarehe 08/03/2023.

Wafanyakazi hawa Wanawake wa TALGWU walimpa heshima hiyo Mh. Mahawanga kama Kiongozi anayejipambanua kama Mama wa wote ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya kazi na makundi yote ya akina Mama na Mabinti kwani amekuwa ni mtu wa kufikika kirahisi na amekuwa kimbilio la Wajasiriamali, akina Mama na Mabinti wengi wa Vikundi hasa kwa uchapakazi wake uliojaa ubunifu.

Mh. Mahawanga amewapongeza sana akina mama hao wa TALGWU kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye jamii na kwa kuunganisha nguvu kuwa na umoja ambao unawaunganisha Mikoa yote mitatu yaani Mkoa wa Ilala, Kinondoni na Temeke.

Sambamba na shughuli zao za kila siku bado akina mama hawa wanapata muda wa kujihusisha na mambo mbalimbali yanayoinua uchumi wa Mwanamke kazini kwa kuwa na Taasisi yao kubwa ya JIJI SACCOS ambayo inawasaidia kupata mikopo yenye riba nafuu sambamba na kujiandalia mazingira mazuri ya kustaafu na kuwaepusha na mikopo isiyorasmi.

Wafanyakazi hawa wa TALGWU walitumia jukwaa hilo kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika nyanja za Miundombinu, Afya, Elimu, Usafiri na Usafirishaji, Uchumi na Fursa. Na wamehaidi kuendelea kumpa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha mazuri haya yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita yanaendelea kuwanufaisha Watanzania wote.

Mh. Mahawanga alipata nafasi ya kuzungumza na Wafanyakazi hao kwa kuendelea kuwasihi tufanye kazi kwa bidii, tuyabeba majukumu yeo kama akina mama na zaidi ya yote tunapopata nafasi tuzitumie kwa weredi, tujipambanue kwani tunaweza tusisubiri kubebwa na tusiwe watu wa kulalamika muda wote.

Vile vile amewaasa Wafanyakazi hao pamoja na majukumu mengi tuliyonayo bado tunawajibu mkubwa wa kuhakikisha tunakomesha huu mmomonyoko wa maadili na vitendo viovu vinavyoendelea kwenye jamii yetu hasa kwa kuwalinda watoto wetu na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kuwataka kila mmoja kuwa balozi kwenye eneo lake na jamii kwa ujumla.

#TishaMama.
#MamaVikoba
#ItazameDarKiutofauti
#KaziIendelee.

WhatsApp Image 2023-03-09 at 16.16.14(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-09 at 16.16.13(1).jpeg
 
Back
Top Bottom