Mbunge Kahama: Wanafunzi waruhusiwe bila Viatu na Sare(Uniform)

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,904
7,817
Anasema elimu itaendelea kukwama kama msisitizo wa unifomu na viatu utaendelea kuwepo. Wazazi ni masikini na hawamudu gharama za kumvisha mwanafunzi...
 
Jaman kama hamjui maana ya vitu kuwekwa mashuleni ni vizuri kuuliza. Hvi itawezekanaje ktk level ya primary wanafunzi ktk karne hii wasivae viatu na UTI yote hii wala uniform? Serikali yenyewe inaona umuhimu Wa kurejesha uniform kwa watumishi wa umma ijekuwa wanafunzi? Hebu apeleke siasa zake huko primary ni uniform viatu na soksi ni lazima sio ombi watoe mambo yao. Mbona mapombe ya kienyeji wanakunywaa weeee!!! Washukuru ningekuwa head hapo wangeona MTU humjali mwanao utamjali nani?
 
Amekomaaa Star tv anawatete wananchi nimestuka sana Anasema mbona Burund wanajiendea tu. Hivi Kishimba si msomi huyu?
 
Mi naona kama huyo mbunge abataka kuwasaidia wananchi wake basi awanunulie uniform na viatu. Akinunua kwa ajili ya maskini tu wasio na uwezo kabisa hata mshahara wake wa miezi mitatu utatosha kumaliza hilo tatizo.
 
Anasema elimu itaendele kukwama ka msisitizo wa unifomu na viatu utaendelea kuwepo.Wazazi ni masikini na hawamudu gharama za kumvisha mwanafunzi

Kwa mara ya kwanza nakubaliana na Mwanasiasa TanZania kwa 100%, angalau kwa mara ya kwanza ktk maisha yangu nimesikia Mwanasiasa TanZania mwenye akili na mwenye kuelewa Dunia inavyokwenda!

Naunga mkono hoja Sare za Shule zipigwe marufuku na mtoto aende shule vyovyote vile alivyo kama na utandio au majani ya kufunika tu sehemu zake siri basi afanye hivyo, kwa kifupi mtoto ni lazima asome na kukosa nguo kusiwe sababu ya mtoto kukosa Elimu, kwani hatutatui tatizo bali tunalizidisha!

Picha chini ni watoto wakiwa darasani wakati wa Ukoloni, Mzungu hakujali mtoto amevaa nini bali cha muhimu kwake ilikuwa ni Mtoto apate Elimu, sasa iweje sisi mtoto masikini wa kimasai ananyimwa elimu kwa kuwa hana uwezo wa kununua Sare?

ba107639.jpg
 
Nimesikia Kishimba akitolea mfano wa enzi ya ukoloni .Ndio maana mikoa imetofautiana sana ki fikra na maendeleo.Sishangai ukizungumzia vyoo ni asilimia 20 %tu Chato 80hawana tunapaswa kuyaendeleza maeneo haya kwa kila hali
 
Huyo mbunge ni dhaifu.

Na hapo ndipo Wazungu na watu mabara mengine kama Asia walipotuzidi sisi Waafrika, kwenye AKILI, yaani uwezo kujua ni nini muhimu ktk maisha, wote Dunia nzima inakubali kwamba Elimu ndiyo inayomkomboa mtoto ktk kwenye Umaskini sasa iweje mtoto anyimwe Elimu kwa kukosa nguo ya kuvaa ambayo siyo kosa lake kwani mzazi wake hana uwezo wa kununua sasa huyu mtoto afanye nini?

Unamfukuza shule mtoto wa miaka 5 kwa sababu baba yake hana uwezo wa kununua viatu hapo unamuadhibu nani sasa? Na halafu kesho panya road wakifunga mitaa kuanza kubaka na kuibia watu tunalalamika kwamba Serikali haitengenezi ajira utatengeza vipi ajira wakati mtoto anafukuzwa shule kwa sababu tu hana viatu?

Ili Afrika tuweze kuendelea tunahitaji watu wenye uwezo wa kufikiria na kuoanisha uhalisia kama Mbunge Kishimba vinginevyo tutaishia kutumwa na kunyanyaswa na wageni maisha yetu yote, na ndiyo maana leo hii tuko tayari kufa majini tukikimbilia Ulaya kwa sababu huku kwetu hakuna fursa, mtoto ananyimwa Elimu kwa kukosa nguo tu?!
 
Anasema elimu itaendele kukwama ka msisitizo wa unifomu na viatu utaendelea kuwepo.Wazazi ni masikini na hawamudu gharama za kumvisha mwanafunzi

Kumbe na wewe umemsikia wangeruhusu kupiga simu ningemwaibisha huyo mzee uelewa wake ni mdogo sasa wasipovaa uniform tutwatambua vipi ni wanafunzi pia jukumu la mzazi litakuwa ni lipi ? itakuwaje watoto wa matajiri wakija na suti ? sijajua uwezo na elimu ya kishimba mpka ashauri uniform ziondolewe kwa upande wa ajira nimekubali wazo lake kwamba watu hawahitaji vyeti bali ujuzi wa kazi husika.
 
miaka ya 80 Marufuku iliwekwa mkoa wa Kilimanjaro wanafunzi kuvaa kobazi za matairi hizi za kimasai. Ndipo zikapata jina,,, raiooo ,,Regional Education Officer,,REOs nchi nzima walitakiwa kuhakikisha wanafunzi wanavaa raba au viatu sio peku wala raio.Kahama wasikubali upuuuzi wa peku cheap politics
 
Kumbe na wewe umemsikia wangeruhusu kupiga simu ningemwaibisha huyo mzee uelewa wake ni mdogo sasa wasipovaa uniform tutwatambua vipi ni wanafunzi pia jukumu la mzazi litakuwa ni lipi ? itakuwaje watoto wa matajiri wakija na suti ? sijajua uwezo na elimu ya kishimba mpka ashauri uniform ziondolewe kwa upande wa ajira nimekubali wazo lake kwamba watu hawahitaji vyeti bali ujuzi wa kazi husika.

Kabla ya kuangalia uwezo wa Elimu wa Kishimba inabidi uangalie uwezo wako wa kielimu kwanza!
Kama Wazungu pia ambao ndio waliomuelimisha baba, babu, bibi, mama yako wangesema ni lazima kwanza wawe na sare ndiyo waje shule kusoma wewe leo hii si ajabu ungekuwa umeshakufa kwa maana ungezaliwa wazazi ambao wasingekuwa na elimu, lkn kwa kuwa Wazungu wana akili waliwaruhusu wazazi wako waje kusoma hata na lubega tu na wengine majani kuficha sehemu za siri ili waelimike leo hii wewe baada ya kufaidi matunda ya wazee wako ambao walienda shule bila ya nguo unaona mtoto wa Kitanzania masikini ambaye mzazi wake hana uwezo na wengine ni yatima wanalelewa na dada na kaka zao walio chini ya miaka 15 wanyimwe Elimu kwa kukosa tu sare za shule!

Huu ni ubinafsi wa hali ya juu na watu kama ninyi ndio wa kwanza kanisani na misikitini kwenye Ibada wakati hamna hata chembe ya utu!
 
Kukimbia tatizo sio njia nzuri na sahihi katika wigo wa utatuzi wa matatizo kwa hiyo watoto kuvaa viatu na uniform lisiwe suala la mashauriano iwe lazima wadau wote wanaohusika including wazazi wahakikishe linatekelezeka mengine mbele kwa mbele..................................
 
Ukizingatia ada na michango imefutwa wazazi wahimizwe kuwavesha watoto wao. Viatu ama raba huzuia ajali.Wakoloni walitoa viatu soksi na unifom. Tazama picha ya mjumbe utaona baadhi wana uniform,wengine vifua wazi hao wanasubiri kukamilika wapewe. Kuna mamo mengi ya hovyo wazazi wanagharimika km ngoma unyago, uganga nk.
 
Kuvaa uniform ni rahisi kuliko.kutovaa umiform!! Jaribu kupiga hesabu mara ngapi katika mwaka mmoja mtoto atajikata na kigae ama kujikwaa na kuoka ngozi katika kidole kwa sababu hakuvaa viatu. Kiasi gani itagharimu katika matibabu yake kwa sababu tu umeepuka kununuwa raba za 5000.

Huu si wakati tena wa quantity katika elimu zetu, umefika wakati tutizame quality ya elimu inayotolewa. Serikali ianatakiwa ikae chini ijiulize inakuwaje mzee anashindwa kumiliki uniforms za watoto wake, chanzo ni nini? Ukimruhusu bila ya uniforms kuja shule, una uhakika gani kama amekula juzi jana na leo yake.

Shule ni taasisi ya mafunzo kwa ajili ya maisha ya baadae. Ikiwa utakuja shule huna viatu, jee ofisini utakwenda bila viatu pia? Ikiwa waziri anataka waruhusiwe watoto waende shule bila viatu, kwa nini waziri huyu huyu hazumgumzii kuruhusiwa mawaziri kwenda maofisini kwa basikeli au kwa Vitz na IST?

Inasikitisha kuwatumia watoto kama chambo katika kutafuta utukufu. Serikali ina wajibu wa kuwasaidia watu waliokuwa hawajiwezi
 
Naunywaji wa pombe pia
Ukizingatia ada na michango imefutwa wazazi wahimizwe kuwavesha watoto wao. Viatu ama raba huzuia ajali.Wakoloni walitoa viatu soksi na unifom. Tazama picha ya mjumbe utaona baadhi wana uniform,wengine vifua wazi hao wanasubiri kukamilika wapewe. Kuna mamo mengi ya hovyo wazazi wanagharimika km ngoma unyago, uganga nk.
.
 
Na hapo ndipo Wazungu na watu mabara mengine kama Asia walipotuzidi sisi Waafrika, kwenye AKILI, yaani uwezo kujua ni nini muhimu ktk maisha, wote Dunia nzima inakubali kwamba Elimu ndiyo inayomkomboa mtoto ktk kwenye Umaskini sasa iweje mtoto anyimwe Elimu kwa kukosa nguo ya kuvaa ambayo siyo kosa lake kwani mzazi wake hana uwezo wa kununua sasa huyu mtoto afanye nini?

Unamfukuza shule mtoto wa miaka 5 kwa sababu baba yake hana uwezo wa kununua viatu hapo unamuadhibu nani sasa? Na halafu kesho panya road wakifunga mitaa kuanza kubaka na kuibia watu tunalalamika kwamba Serikali haitengenezi ajira utatengeza vipi ajira wakati mtoto anafukuzwa shule kwa sababu tu hana viatu?

Hivi unajua mazingira ya vyoo vya shule za msingi serikali,hata masomo hawatamaliza wataishia kuugua na kushindwa Masomo.Huyu mbunge anatakiwa atafakari vizuri
 
Zama za kusoma bila viatu zimeshapita. Hata kama sio viatu imara lakini sio sawa na miguu mitupu.
 
Ndiyo shida ya kupeleka bungeni watu wa darasa la saba tena la kulazimishwa. Biashara iwe biashara na bunge liwe ni mahala pa watu wenye intellectual ability ya kutoa miongozo yenye macho kwa maendeleo ya taifa.

Hii inadhihirisha ni jinsi gani ccm imezidi kudunisha maisha ya Watanzania kiasi cha kuturudisha miaka mingi sana nyuma ambako tulisha toka. Hivi ni wanafunzi wangapi hawaendi shule kwa sababu ya kukosa sare na viatu? Hili bunge sasa linahalaisha umaskini wa fikra na ujinga wa kutokujali hata faida za usafi binafsi na sare katika elimu ya watoto.

Wazazi wenyewe wanajua. Kama hana uwezowa kununua nguo mbili za mtoto, basi hiyo moja ni uniform ya shule.

Haya ndiyo matokeo ya ccm kupeleka mibunge isiyo kwenda shule.
 
Back
Top Bottom