Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,140
Mbunge Joshua Nassari awaonya Viongozi wa dini Kuacha kuwasafisha Mafisadi wanaomwaga Fedha Makanisani na Misikitini kila Kukicha...!!
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, amewataka viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwasafisha watu wanaohusika na vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia madhabahu ya makanisa na misikiti kwani kufanya hivyo ni kubariki dhambi.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Meru, Usharika wa Emmanuel, uliopo Kata ya Mororoni, wilayani Arumeru katika harambee ya ujenzi wa kanisa jipya.
Mbunge huyo alisema watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi na madaraka yao wamekuwa wakitumia makanisa na misikiti kuchangisha mamilioni ya fedha.
"Hatujui hizo pesa zao zimetoka wapi? Hizo ni pesa chafu na za wizi. Nawaomba viongozi wa dini na wananchi msishiriki hiyo dhambi, ni bora tujenge makanisa na misikiti kwa fedha za kuokoteza kuliko fedha chafu," alisema Nassari.
Nassari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, amewataka viongozi hao kuacha tabia ya kuwasafisha na kuwawekea mikono viongozi hao wezi.
Hata hivyo Mkuu wa Jimbo la Kusini, KKKT Dayosisi ya Meru, Zelote Palangyo, alisema kuwa utamaduni wa kumjengea Mungu sehemu ya kumwabudia ni alama ya kuonyesha uthamani na umuhimu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ernest Mbise, alisema ujio wa mbunge huyo umetoa hamasa katika uchangiaji wa shughuli hiyo muhimu ya ujenzi wa kanisa.
Jumla ya sh milioni 101 zilichangishwa pamoja na mifugo, ikiwemo ng'ombe, mbuzi na kuku.
----Tanzania Daima
Nassari, chadema haisadiwi na CDU? na mialiko ya Katibu Mkuu wenu USA hivi karibuni ilifadhiliwa na nani?
Au dhambi ni kutoa tu na si kupokea kutoka kwenye taasisi za kidini?
Mim ninaunga Mkono Viongozi wa Kisiasa kutowa misaada yao kupelekaMkuu Mzizi Mkavu hii ni Hakika kabisa ni aibu na kumtukana Mungu (kukufuru) kwa Kanisa kujengwa na Fedha za Majambazi na mafisadi (reputed Fisadis) huku likifahamu fika . Ikumbukwe hata vile vipande thelathini alivyo hongwa Yuda Iskariot ili Kumsaliti Yesu alivyo virudisha Hekaluni baada ya kugundua kwamba amemsaliti mtu asiye na hatia wale Makuhani na wazee wa Baraza walikataa zisiingizwe kwenye Akiba ya Hekalu kwa sababu nifedha za damu (haramu) bali zikanunue eneo la Makaburi (tena ya kuzikia Wageni (kafiri) siyo wayahudi)
kiongozi yeyote wadini ya Kikristo anaye mkumbatia Fisadi,Mwizi,Muuaji,mtu mwenye visasi asiyetubu na kumshirikisha katika ibada
takatifu na kupokea matoleo yake ni MPINGA KRISTO
Mim ninaunga Mkono Viongozi wa Kisiasa kutowa misaada yao kupeleka
Makanisani na Misikitini kwa sababu ya hiyari yao kusaidia Dini Sio kuomba kura hapo sipo pamoja nao. Kwa sababu Serikali haina Dini
ila Viongozi wa Serikali wanazo Dini zao sasa huwezi kumkataza mtu mwenye mapenzi ya dini kutowa misaada kwa kisingizio eti anaomba apewe kura wakati wa uchaguzi hayo maneno ni ya viongozi wa kisisa tu.
Mbunge Joshua Nassari awaonya Viongozi wa dini Kuacha kuwasafisha Mafisadi wanaomwaga Fedha Makanisani na Misikitini kila Kukicha...!!
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, amewataka viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwasafisha watu wanaohusika na vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia madhabahu ya makanisa na misikiti kwani kufanya hivyo ni kubariki dhambi.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Meru, Usharika wa Emmanuel, uliopo Kata ya Mororoni, wilayani Arumeru katika harambee ya ujenzi wa kanisa jipya.
Mbunge huyo alisema watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi na madaraka yao wamekuwa wakitumia makanisa na misikiti kuchangisha mamilioni ya fedha.
"Hatujui hizo pesa zao zimetoka wapi? Hizo ni pesa chafu na za wizi. Nawaomba viongozi wa dini na wananchi msishiriki hiyo dhambi, ni bora tujenge makanisa na misikiti kwa fedha za kuokoteza kuliko fedha chafu," alisema Nassari.
Nassari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, amewataka viongozi hao kuacha tabia ya kuwasafisha na kuwawekea mikono viongozi hao wezi.
Hata hivyo Mkuu wa Jimbo la Kusini, KKKT Dayosisi ya Meru, Zelote Palangyo, alisema kuwa utamaduni wa kumjengea Mungu sehemu ya kumwabudia ni alama ya kuonyesha uthamani na umuhimu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ernest Mbise, alisema ujio wa mbunge huyo umetoa hamasa katika uchangiaji wa shughuli hiyo muhimu ya ujenzi wa kanisa.
Jumla ya sh milioni 101 zilichangishwa pamoja na mifugo, ikiwemo ng'ombe, mbuzi na kuku.
----Tanzania Daima
rudia hayo maneno leoNi kweli kuwa Lowassa ni mchafu (refer kashfa za Richmond etc) na speed zake makanisani na misikitini akiwa amebeba na kugawa pesa chafu akiutafuta urais kwa bei yoyote ni ishara ya kujiswafi huku akijibanza madhabauni.
Well said Joshua Nassari.