Mbunge Joshua Nassari awaonya Viongozi wa dini Kuacha kuwasafisha Mafisadi wanaomwaga Fedha Makanisa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,267
33,039
Mbunge Joshua Nassari awaonya Viongozi wa dini Kuacha kuwasafisha Mafisadi wanaomwaga Fedha Makanisani na Misikitini kila Kukicha...!!

MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, amewataka viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwasafisha watu wanaohusika na vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia madhabahu ya makanisa na misikiti kwani kufanya hivyo ni kubariki dhambi.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Meru, Usharika wa Emmanuel, uliopo Kata ya Mororoni, wilayani Arumeru katika harambee ya ujenzi wa kanisa jipya.

Mbunge huyo alisema watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi na madaraka yao wamekuwa wakitumia makanisa na misikiti kuchangisha mamilioni ya fedha.
LOWASSA2.jpg

“Hatujui hizo pesa zao zimetoka wapi? Hizo ni pesa chafu na za wizi. Nawaomba viongozi wa dini na wananchi msishiriki hiyo dhambi, ni bora tujenge makanisa na misikiti kwa fedha za kuokoteza kuliko fedha chafu,” alisema Nassari.

Nassari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, amewataka viongozi hao kuacha tabia ya kuwasafisha na kuwawekea mikono viongozi hao wezi.

Hata hivyo Mkuu wa Jimbo la Kusini, KKKT Dayosisi ya Meru, Zelote Palangyo, alisema kuwa utamaduni wa kumjengea Mungu sehemu ya kumwabudia ni alama ya kuonyesha uthamani na umuhimu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ernest Mbise, alisema ujio wa mbunge huyo umetoa hamasa katika uchangiaji wa shughuli hiyo muhimu ya ujenzi wa kanisa.
Jumla ya sh milioni 101 zilichangishwa pamoja na mifugo, ikiwemo ng’ombe, mbuzi na kuku.

----Tanzania Daima
 
Nassari, chadema haisadiwi na CDU? na mialiko ya Katibu Mkuu wenu USA hivi karibuni ilifadhiliwa na nani?

Au dhambi ni kutoa tu na si kupokea kutoka kwenye taasisi za kidini?
 
Mbunge Joshua Nassari awaonya Viongozi wa dini Kuacha kuwasafisha Mafisadi wanaomwaga Fedha Makanisani na Misikitini kila Kukicha...!!

MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, amewataka viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwasafisha watu wanaohusika na vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia madhabahu ya makanisa na misikiti kwani kufanya hivyo ni kubariki dhambi.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Meru, Usharika wa Emmanuel, uliopo Kata ya Mororoni, wilayani Arumeru katika harambee ya ujenzi wa kanisa jipya.

Mbunge huyo alisema watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi na madaraka yao wamekuwa wakitumia makanisa na misikiti kuchangisha mamilioni ya fedha.
LOWASSA2.jpg

"Hatujui hizo pesa zao zimetoka wapi? Hizo ni pesa chafu na za wizi. Nawaomba viongozi wa dini na wananchi msishiriki hiyo dhambi, ni bora tujenge makanisa na misikiti kwa fedha za kuokoteza kuliko fedha chafu," alisema Nassari.

Nassari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, amewataka viongozi hao kuacha tabia ya kuwasafisha na kuwawekea mikono viongozi hao wezi.

Hata hivyo Mkuu wa Jimbo la Kusini, KKKT Dayosisi ya Meru, Zelote Palangyo, alisema kuwa utamaduni wa kumjengea Mungu sehemu ya kumwabudia ni alama ya kuonyesha uthamani na umuhimu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ernest Mbise, alisema ujio wa mbunge huyo umetoa hamasa katika uchangiaji wa shughuli hiyo muhimu ya ujenzi wa kanisa.
Jumla ya sh milioni 101 zilichangishwa pamoja na mifugo, ikiwemo ng'ombe, mbuzi na kuku.

----Tanzania Daima

Mkuu Mzizi Mkavu hii ni Hakika kabisa ni aibu na kumtukana Mungu (kukufuru) kwa Kanisa kujengwa na Fedha za Majambazi na mafisadi (reputed Fisadis) huku likifahamu fika . Ikumbukwe hata vile vipande thelathini alivyo hongwa Yuda Iskariot ili Kumsaliti Yesu alivyo virudisha Hekaluni baada ya kugundua kwamba amemsaliti mtu asiye na hatia wale Makuhani na wazee wa Baraza walikataa zisiingizwe kwenye Akiba ya Hekalu kwa sababu nifedha za damu (haramu) bali zikanunue eneo la Makaburi (tena ya kuzikia Wageni (kafiri) siyo wayahudi)

kiongozi yeyote wadini ya Kikristo anaye mkumbatia Fisadi,Mwizi,Muuaji,mtu mwenye visasi asiyetubu na kumshirikisha katika ibada takatifu na kupokea matoleo yake ni MPINGA KRISTO
 
Ni kweli kuwa Lowassa ni mchafu (refer kashfa za Richmond etc) na speed zake makanisani na misikitini akiwa amebeba na kugawa pesa chafu akiutafuta urais kwa bei yoyote ni ishara ya kujiswafi huku akijibanza madhabauni.

Well said Joshua Nassari.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzizi Mkavu hii ni Hakika kabisa ni aibu na kumtukana Mungu (kukufuru) kwa Kanisa kujengwa na Fedha za Majambazi na mafisadi (reputed Fisadis) huku likifahamu fika . Ikumbukwe hata vile vipande thelathini alivyo hongwa Yuda Iskariot ili Kumsaliti Yesu alivyo virudisha Hekaluni baada ya kugundua kwamba amemsaliti mtu asiye na hatia wale Makuhani na wazee wa Baraza walikataa zisiingizwe kwenye Akiba ya Hekalu kwa sababu nifedha za damu (haramu) bali zikanunue eneo la Makaburi (tena ya kuzikia Wageni (kafiri) siyo wayahudi)

kiongozi yeyote wadini ya Kikristo anaye mkumbatia Fisadi,Mwizi,Muuaji,mtu mwenye visasi asiyetubu na kumshirikisha katika ibada

takatifu na kupokea matoleo yake ni MPINGA KRISTO
Mim ninaunga Mkono Viongozi wa Kisiasa kutowa misaada yao kupeleka

Makanisani na Misikitini kwa sababu ya hiyari yao kusaidia Dini Sio kuomba kura hapo sipo pamoja nao. Kwa sababu Serikali haina Dini

ila Viongozi wa Serikali wanazo Dini zao sasa huwezi kumkataza mtu mwenye mapenzi ya dini kutowa misaada kwa kisingizio eti anaomba apewe kura wakati wa uchaguzi hayo maneno ni ya viongozi wa kisisa tu.
 
Ni kweli kabisa unachozungumza Mzizi Mkavu lakini ndo maake nilikuwa very specific kwenye mchango wangu nikijielekeza kwenye Dini ya Kikristo kwani inakataza kabisa kutoa sadaka au matoleo yenye kasoro. Kwa mujibu wa Dini hii hata unapokuwa ukitaka kutoa sadaka na ukakumbuka kwamba kuna mtu mmekosana unatakiwa uiache pembeni bila kutoa sadaka hiyo uende ukapatane na mgovi wako kwanza ndipo urudi kuendelea kutoa sadaka yako.

Kinachofanyika sasa watu wanakusanya fedha kwa malengo maalum bila kujali zinatoka wapi,kwanani na kupeleka Makanisani ndo maake unaona hata ukiingia kwenye baadhi ya Makanisa yananuka dhambi,udhalilishaji watoto,wizi,ushirikina ni kwasababu yamejengwa juu ya laana na vilio vya wanyonge.

Kuna watu wanastahili kutuomba radhi watanzania kwa kutuibia bila kujiumauma maneno na warudishe mara nne kama Zakayo mtoza ushuru alivyofanya baada ya kugundua makosa yake kile walicho kiiba kabla ya kuanza kutudanganya na kutughilibu kwa vimichango makanisani
 
Cha kuudhi katika sakata hili,wapo ambao UTII wao upo si kwa sababu wanaamin itikadi au maono ya viongozi wao bali kwa sababu MATUMBO yao na mifuko yanawategemea watu hawa.hivyo wamekua watetezi wa kimaslai zaid,siku minofu hiyo ikikatwa watatafuta mahali pengine pa kuegememea
 
Basi muweni na mioyo safi..enendeni katika unyenyekevu, utii na heshima kwa watesi- watawala wenu, ili kweli yake kwamba atawainua na kuwaweka juu katika kiti cha enzi ipate kutimilizika! Kazaneni kuhubiri ukweli, himizaneni ninyi kwa ninyi kuuishi ukweli...wataibuka watu miongoni mwa watesi wenu nao wataihubiri hiyo kweli ilihali mioyo yao imejaa unafiki na chuki, na roho mbaya, na wizi na roho ya kifisadi...msivunjike moyo kwa sababu hawatadumu wala walinenalo nalo halitadumu...Kuweni na mioyo ya subira na tumaini lililo kuu mioyoni mwenu. Atokeapo mmoja kati yenu kuwa na roho ya usaliti msisite kuonyana, akikili na kuiacha roho ya kisaliti mbakisheni kati yenu, aking'ang'ana katika usaliti muwekeni kando,msimpe nafasi kuwaumizeni. Jihadhalini na tamaa ya vitu na mali za dunia hii kwa sababu zaweza kuwafarakanisha mkakosa kuelewana, atakayebahatika kuwa na mali na utajiri na asijivune navyo wala asijione ana upekee kati yenu, atabarikiwa sana kama atatumia sehemu ya utajiri wake kuihubiri na kuiishi hiyo kweli. Pendaneni, na wakati wote wa kutimiza majukumu yenu kama mtakavyogawana, Shirikianeni. Mmebarikiwa tofauti na mna uwezo tofauti, heshimianeni katika hilo na asitokee mmoja kati yenu akajiona bora kuliko mwingine. Nawatakieni kila lililo ha heri katika safari yenu hii ngumu. DUMUNI KATIKA KWELI NA UMOJA.
 
Mbunge Joshua Nassari awaonya Viongozi wa dini Kuacha kuwasafisha Mafisadi wanaomwaga Fedha Makanisani na Misikitini kila Kukicha...!!

MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, amewataka viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwasafisha watu wanaohusika na vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia madhabahu ya makanisa na misikiti kwani kufanya hivyo ni kubariki dhambi.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Meru, Usharika wa Emmanuel, uliopo Kata ya Mororoni, wilayani Arumeru katika harambee ya ujenzi wa kanisa jipya.

Mbunge huyo alisema watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi na madaraka yao wamekuwa wakitumia makanisa na misikiti kuchangisha mamilioni ya fedha.
LOWASSA2.jpg

"Hatujui hizo pesa zao zimetoka wapi? Hizo ni pesa chafu na za wizi. Nawaomba viongozi wa dini na wananchi msishiriki hiyo dhambi, ni bora tujenge makanisa na misikiti kwa fedha za kuokoteza kuliko fedha chafu," alisema Nassari.

Nassari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, amewataka viongozi hao kuacha tabia ya kuwasafisha na kuwawekea mikono viongozi hao wezi.

Hata hivyo Mkuu wa Jimbo la Kusini, KKKT Dayosisi ya Meru, Zelote Palangyo, alisema kuwa utamaduni wa kumjengea Mungu sehemu ya kumwabudia ni alama ya kuonyesha uthamani na umuhimu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ernest Mbise, alisema ujio wa mbunge huyo umetoa hamasa katika uchangiaji wa shughuli hiyo muhimu ya ujenzi wa kanisa.
Jumla ya sh milioni 101 zilichangishwa pamoja na mifugo, ikiwemo ng'ombe, mbuzi na kuku.

----Tanzania Daima

Mbunge mla rushwa kutoka CDM...
 
Ni kweli kuwa Lowassa ni mchafu (refer kashfa za Richmond etc) na speed zake makanisani na misikitini akiwa amebeba na kugawa pesa chafu akiutafuta urais kwa bei yoyote ni ishara ya kujiswafi huku akijibanza madhabauni.

Well said Joshua Nassari.
rudia hayo maneno leo

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom