Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,082
Mbunge Joshua Nassari awaonya Viongozi wa dini Kuacha kuwasafisha Mafisadi wanaomwaga Fedha Makanisani na Misikitini kila Kukicha...!!
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, amewataka viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwasafisha watu wanaohusika na vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia madhabahu ya makanisa na misikiti kwani kufanya hivyo ni kubariki dhambi.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Meru, Usharika wa Emmanuel, uliopo Kata ya Mororoni, wilayani Arumeru katika harambee ya ujenzi wa kanisa jipya.
Mbunge huyo alisema watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi na madaraka yao wamekuwa wakitumia makanisa na misikiti kuchangisha mamilioni ya fedha.
Hatujui hizo pesa zao zimetoka wapi? Hizo ni pesa chafu na za wizi. Nawaomba viongozi wa dini na wananchi msishiriki hiyo dhambi, ni bora tujenge makanisa na misikiti kwa fedha za kuokoteza kuliko fedha chafu, alisema Nassari.
Nassari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, amewataka viongozi hao kuacha tabia ya kuwasafisha na kuwawekea mikono viongozi hao wezi.
Hata hivyo Mkuu wa Jimbo la Kusini, KKKT Dayosisi ya Meru, Zelote Palangyo, alisema kuwa utamaduni wa kumjengea Mungu sehemu ya kumwabudia ni alama ya kuonyesha uthamani na umuhimu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ernest Mbise, alisema ujio wa mbunge huyo umetoa hamasa katika uchangiaji wa shughuli hiyo muhimu ya ujenzi wa kanisa.
Jumla ya sh milioni 101 zilichangishwa pamoja na mifugo, ikiwemo ngombe, mbuzi na kuku.
----Tanzania Daima