barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" ameamua kutii kiu ya mashabiki wake wa mziki wa "kufokafoka" kwa kutoka na Wimbo mpya wa "Freedom".Wimbo huo wenye mahadhi ya hip hop umerekodiwa na studio ya MJ Records ya jijini Dsm
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na kuwa busy na pilikapilika za kampeni,Mh Sugu ameamua kutoa wimbo huo kutii kiu ya mashabiki wake wa toka miaka ya 1990.Akiongea katika eneo la Ununio alikokuwa anarekodi video ya wimbo huo,Sugu alisema "Nimekuwa kimya kwa muda mrefu sababu ya mambo ya kampeni na siasa,Baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka jana nilishinda ubunge wa Mbeya Mjini,nilichaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge yoyote wa Tanzania.Kwa heshima ya watu wangu wa muziki ninawaletea single ya wimbo huu wa Freedom"
Video ya wimbo huo wa Sugu inaandaliwa na kijana Hanscana ambaye ni moja kati ya wazalishaji wadogo wa video nchini Tanzania.Mandhali ya video hiyo imechukuliwa katika jiji la Dsm na itashirikisha watu wengi maarufu kama Mbunge wa Mikumi Prof J,Master J,Shaa na Roma Mkatoliki.
Baadhi ya picha za Video hiyo iliyochukuliwa ktk maeneo ya viwanja vya Golf na majengo ya Ufukweni mwa jiji la Dsm