barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Leo nilikuwa napita kwenye "wall" ya bwana mdogo Ezekiel Maige,mbunge wa Msalala na Waziri wa Zamani wa Maliasili na Utalii.
Nikakuta mjadala,mjadala ulioasisiwa na mwanachi mmoja akimkosoa Maige kuwa hajafanya lolote katika jimbo la Msalala sababu kwa miaka yote aliyokaa bungeni eneo la Isaka halina huduma ya maji hata kwa kiwango cha visima.
Katika mjadala huo,akajitokeza mwananchi mmoja,akawa anahoji,inakuwaje kuwa eneo ambalo kwa miaka 50 hawajawahi kuwa na huduma ya maji ya uhakika na bado wanachagua chama hicho na watu walewale?Wakati kuna maeneo maji yanafika mpaka mlangoni lakini wanakitupilia mbali chama dola katika uchaguzi.
Bila kufikiri,Maige alimshambulia sana mwananchi yule kwa kumuita "mchaga",ambao JPM kaamua kupambana nao sbb kwa miaka mingi "waliitafuna" nchi hii.Kuanzia CRDB mpaka TRA walijazana wao tu.Lakini sasa JPM kaamua "kuwabana" na "kuwakumbuka" watu wa maeneo mengine.
Kwa kweli mjadala huu ulinisikitisha,umeonyesha jinsi ambavyo viongozi aina ya Maige wasivyoweza kustahimili maswali na mijadala na kujificha katika "kete" ya ukabila na ukanda.Lakini ni muda sasa hili suala lijulikane,kwamba ni kweli hao wanaoitwa "wachaga" waliitafuna nchi hii kwa muda mrefu?
Ina maana kwa sasa kuna hatua zinachukuliwa kuhakikisha hawa wa kabila hili wanadhibitiwa?Yeye Maige kama mbunge na waziri wa zamani,aliwahi kuchukua hatua gani kuhakikisha hawa "wachaga" wanaojipendelea,wanathibitiwa?
Kwa aina hii ya mtazamo na mjadala toka kwa mbunge na kiongozi aina ya Maige,ni wazi sasa,hatuko salama sana kuelekea katika ubaguzi na utengano unaotokana na mbegu za ukabila na ukanda.Maige ameamua kusema,kuna wengine wasiosema na kutekeleza kimyakimya...Ukabila na hisia za ukabila ni sumu kwa umoja wa kitaifa.