MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wale wanaojinasibisha hapa Jamiiforums kama wazalendo wakati ni wanafiki, ingekuwa ni vizuri wakamsikiliza kwa makini Esther Matiko ili wajifunze namna ambavyo wapinzani wanaweza kutoa hoja kwa serikali, kuisimamia na kutoa ushauri.
Huyu ni kati ya wabunge wachache wa upinzani ambao siyo wanafiki.
Ni mbunge ambaye anafundisha, anakosoa katika msingi wa nguvu za hoja, anashauri katika msingi wa kujenga na anatoa shukrani katika msingi wa haki.
Hoja zake niza kujenga taifa na siyo kubeza viongozi au kubomoa taifa kama walivyo wanafiki waliojivika kofia za upinzani ambapo na wengine wapo hapa Jamiiforums.
Wale wanafiki ni vizuri wakajifunza kutoka kwa Esther Matiko.
Ameuchambua Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17 katika maeneo ya hali ya kiuchumi na utekelezaji wake hasa kwa kuangalia mafanikio ya Mpango kama huo wa mwaka 2014/15.
Amechambua ugharamiaji wa mpango hasa kwenye vyanzo vya mapato ya ndani na vihatarishi vya utekelezaji wa mpango.
Alimalizia mchango wake kwa kumshukuru Mwigulu Nchemba kwa kuonyesha uzalendo katika kazi zake bila kujali itikadi ya vyama vya siasa.
Ninaamini Rais Magufuli anahitaji sana wabunge wa aina ya Esther Matiko ili waisaidie serikali yake pale inatoka nje ya mstari iweze kukumbushwa na kurudi katika mstari kwa faida ya ustawi wa taifa letu.
Wananchi wa Jimbo la Tarime Mjini hawakufanya makosa katika kulisaidia taifa kwa kutuletea Esther Matiko kama Mbunge.
Naomba nikupe nafasi ili uweze kumsikiliza kwenye video kwa makini.