Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ametoa zaidi ya tani mbili za sukari kwenye misikiti iliyopo katika Jimbo la Buchosa ikiwa ni sehemu ya sadaka kwa waumini wa dini ya Kiislamu wanaoendelea na mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sukari hiyo imegawanywa na Katibu wa Mbunge, Julias Butogwa kwenye misikiti mbalimbali kwa niaba ya Shigongo.
Amesema Shigongo amefanya hivyo kwa wananchi wa jimbo hilo ili iwasaidie kwa matumizi mbalimbali wakati wa mfungo.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wa Misikiti ya Kanyala, Mbugani na Luchili wamepongeza hatua ya Mbunge Shigongo, kwa kutoa msaada huu ambao utawasaidia kwa kiasi kikubwa waumini wao.
Wamesema wanamwombea heri katika majukumu yake ya kuwatumikia Wanabuchosa na Watanzania kwa jumla.