Mbunge Ditopile aongoza dua ya kumuombea Rais Samia

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
MBUNGE wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amejumuika pamoja na viongozi wa Dini, Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Wananchi mbalimbali katika Dua maalum aliyoiandaa ya kuliombea Taifa letu na Rais Samia Suluhu Hassan sambamba na kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa yeye pia.

Dua hiyo maalumu imefanyika katika viwanja vya Kitengo Bicha wilayani Kondoa kilipo kituo cha kulelea Watoto Yatima na wenye uhitaji ambapo Mbunge Ditopile amewasihi watanzania na wananchi kwa ujumla kumuombea Rais Samia kwani tangu ameingia madarakani ameonyesha dhamira yake ya kuiletea maendeleo Nchi yetu.

" Niwashukuru kwa kutenga muda wenu kukubali kushiriki Dua hii Maalum ya kuliombea Taifa letu na Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ombi langu kwenu tuendelee kumuunga mkono Kiongozi wetu ambaye hakika mambo aliyoyafanya ndani ya kipindi cha Miezi 14 Madarakani ni makubwa hivyo anahitaji kutiwa moyo.

"Niwaombe kuiunga mkono Serikali yenu ya awamu ya sita ambayo imeendelea kuongoza Nchi yetu kwa amani na sisi leo tunafanya Dua hapa kukiwa na utulivu huku tukiendesha shughuli zetu za kiimani kwa amani na utulivu, " Amesema Mbunge Ditopile.

Ditopile pia ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kushiriki kwa ukamilifu zoezi la Sensa ambalo linatarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu akisisitiza kuwa ushiriki wa wananchi utasaidia Serikali kujua idadi ya wananchi wake katika kupanga bajeti za kuwaletea maendeleo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma amempongeza Mbunge Mariam kwa namna alivyojitoa kuandaa Dua hiyo maalum ya kuiombea Nchi na Rais Samia sambamba na kuandaa futari hiyo.

Amesema tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo huku akizidi kuwaunganisha Watanzania bila kujali tofauti zao za kiimani na vyama.

" Rais Samia kwa kipindi kifupi amefanya kazi kubwa ya kimaendeleo, kutengeneza mahusiano na kutuunganisha kwa pamoja, sisi kama viongozi wa Dini tutaendelea kumuunga mkono, kumuombea ili azidi kuwa na afya njema na kuwatumikia watanzania.

Ni jambo kubwa na la kiimani kuandaa Dua Maalum ya kumuombea Rais Samia na Nchi yetu, nikupongeze sana Mhe Mariam Ditopile kwa upendo huu mkubwa na zaidi kutuandalia futari ya pamoja, hii inaonesha ukomavu wako kama Kiongozi na moyo wa Upendo ulionao," Amesema.
IMG_20220427_200305_471.jpg
IMG_20220427_200305_514.jpg
IMG_20220427_200305_423.jpg
 
Huyu Mbunge humuambii kitu kwa Chifu Hangaya! Sijui ana mafungamano gani huyu na Mheshimiwa! Au ndiyo kujipendekeza kwa Chifu ili ampe na yeye aongeze urefu wa kamba!
 
Simshangai Mariam hata enz za jiwe.zile mada zakuwananga wapinzan wa jiwe alikuwa anapewa yeye na kibajaji

Mambo ya hovyo hupewa yeye na kibajaji enz za jiwe

Sasa anaandaa njia ya kukumbukwa Tena maana utawala ushabadirika

RAIS NCHI HII KWAO CCM N ZAID YA MUNGU

SI MNAMKUMBUKA YULE MWANA CCM ALIYESEMA MUNGU APENDE ASIPENDE LAZMA WASHINDE




Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mtu anaetumia tecno F1 huwa simwamini
Simshangai Mariam hata enz za jiwe.zile mada zakuwananga wapinzan wa jiwe alikuwa anapewa yeye na kibajaji

Mambo ya hovyo hupewa yeye na kibajaji enz za jiwe

Sasa anaandaa njia ya kukumbukwa Tena maana utawala ushabadirika

RAIS NCHI HII KWAO CCM N ZAID YA MUNGU

SI MNAMKUMBUKA YULE MWANA CCM ALIYESEMA MUNGU APENDE ASIPENDE LAZMA WASHINDE




Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mwigulu Nchemba akimpa Pole Mzee John Malecela kwa kufiwa na Mwanae Mwale akatafuta namna ya kuhakikisha hata katika salamu hizi za Msiba anamtaja taja Rais…akajikuta anapost eti anaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kumpa pole Mzee Malecela akamlizia kwa kumtag Rais ili aone

mwingine Mbunge wa viti Maalumu akampongeza Rais kwa kwenda na kurudi salama kutoka Marekani

sasa hivi kujipendekeza, kusema uongo, kuwa chawa, kujitoa akili sio aibu wala fedheha tena
Huyu Mbunge humuambii kitu kwa Chifu Hangaya! Sijui ana mafungamano gani huyu na Mheshimiwa! Au ndiyo kujipendekeza kwa Chifu ili ampe na yeye aongeze urefu wa kamba!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom