Mbunge CUF ‘aibeba’ CCM

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,365
33,004
MBUNGE wa Lindi Mjini, Salum Barwani (CUF) amesema anatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/15 kwa kuwa chama chake hakikushinda uchaguzi mkuu wa urais.

Barwani alisema hayo jana alipozungumza na gazeti hili ofisi kwake baada ya kuwasili jimboni kutoka kwenye Mkutano wa Bunge mjini Dodoma. Aliwataka wananchi wa jimbo lake kutambua kuwa maendeleo hayaji kwa miujiza, wala juhudi zake peke yake, ila yatakuja baada ya kuwa na mshikamano wa pamoja kati ya Serikali ya CCM, wananchi na yeye.

“Ndugu zangu maendeleo ya Lindi hayawezi kupatikana kwa juhudi za mbunge peke yake, bali umoja na mshikamano ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo, mimi peke yangu siwezi kuleta maendeleo kama mnafikiria hivyo basi ni ndoto ya mchana,” alisema.

Mbunge huyo pia alikiri kuwekwa ‘kiti moto’ na baadhi ya wananchi aliokutana nao wakimtuhumu kukaa muda mrefu Dar es Salaam bila kwenda kuwaona.

Mbunge huyo alisema Baraza la Utendaji la Wilaya la CUF lilimwita na kumweka kikao Jumamosi na kumhoji sababu za kutumia muda mwingi Dar es Salaam na kutokwenda kuona wananchi baada ya Bunge la Bajeti.


Soma yote hapa: HabariLeo | Mbunge CUF ‘aibeba’ CCM
 
Leo ndio anagundua kuwa hawezi kuleta maendeleo sio? Wakati wa kuomba kura alisemaje?

Kwanza nani kamwambia kuwa maendeleo yanaletwa na mshikamano? Maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na watu kuwa waadilifu. Tanzania na hasa huko Lindi watu wanashikamana sana (kwenda kwenye ngoma, kwenda kuona wagonjwa hospitali na kwenda kwa waganga nk) lakini mbona bado maendeleo hayaonekani.

Aache 'simple excuses' awe mkali aibane serekali itimize majukumu yake na yeye atimize majukumu yake hata kama wako mbali mbali
 
Back
Top Bottom