Mbunge CUF aanguka Bungeni Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge CUF aanguka Bungeni Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Apr 15, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni habari ya kusikitisha.

  Mbunge aanguka Bungeni

  Habel Chidawali,Dodoma

  MBUNGE wa Viti Maalumu (CUF), Clara Mwatuka jana aliugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa ajili ya matibabu.Mwatuka alipatwa na maswahiba hayo mchana wakati akishiriki semina ya wabunge kuhusu anuani mpya ya makazi na simbo za posta pamoja na teknolojia mpya ya utangazaji.

  Semina hiyo ilikuwa ikifanyika katika Ukumbi wa Pisu Msekwa ndani ya majengo ya bunge ambapo ghalfa mbunge huyo alionekana kulegea na kuhitaji huduma ya haraka.

  Mara kadhaa katika mikutano ya bunge, kumekuwa kukitokea matatizo ya wabunge kuugua ghafla na kukimbizwa hospitali na kwa mara ya mwisho ilikuwa Juni 24 mwaka jana ambapo mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mwanahamisi Kassim Said aliugua ghalfa na kukimbizwa hospitali ambapo alisababisha shughuli za bunge kusimama kwa muda.

  Mmoja wa wahudumu wa zahanati ya bunge ambaye hakupenda kuandikwa jina lake, alisema kuwa mbunge huyo alifikishwa katika kituo hicho na kuonekana kuwa anahitaji msaada zaidi na hivyo akakimbizwa hospitali ya mkoa.
  "Mheshimiwa tumempokea hapa, lakini hali yake haikuwa mbaya sana ila tuliamua kumkimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake,''alisema mhudumu huyo.

  Uongozi wa wa hospitali ya mkoa haukupatikana kuzungumzia suala hilo ingawa simu zao za mkononi ziliita bila ya majibu.
  Hata hivyo, mmoja wa wauguzi hospitalini hapo ambaye alisema kuwa si msemaji, aliliambia gazeti hili kuwa walimpokea mbunge huyo kutoka kituo cha bunge na kwamba alikuwa amewekwa mapumziko katika wodi maalumu hospitalini hapo.

  Mwananchi Jumapili ilipata bahati ya kuzungumza na Mwatuka moja kwa moja kwa njia ya simu akiwa hospitalini hapo ambapo alieleza kuwa hali yake si mbaya sana.

  "Nashukuru kwa kunipa pole, ukweli ni kwamba naendelea vizuri, lakini bado niko chini ya uangalizi wa madaktari si unajua kuingia ni rahisi kutoka lazima itachukua muda,''alisema Mwatuka kwa sauti ya chini.

  Alipotakiwa kuelezea hasa nini kinachomsumbua mbunge huyo alisema "Kweli sijui, nahisi inaweza kuwa ni presha (shinikizo la damu) lakini nasubiri madaktari waseme wenyewe.''

  Hata hivyo, mbunge huyo alieleza kuwa amekuwa akisumbuliwa na presha pamoja na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu jambo linalomfanya mara zote kuwa na tahadhari kubwa.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Pole sana mb wa cuf.
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kuna haja ya kuweka utamaduni wa kucheki afya kila wakati
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hivi hawa Wabunge kila wakati kabla ya Vikao Vya Bunge kuanza wanachekiwa Afya zao haswa Moyo na Pressure?

  Kwasababu bunge linasisimua Mwili, na kama ni mchapakazi linaweza kukata Moyo Usifanye kazi

  Kwahiyo hiyo Hospitali ya Dodoma nadhani sio sawasawa na zingine kama Bugando, Temeke, Mbeya, zisizo na vifaa na

  Madaktari bingwa wa kupima na kuchunguza Mioyo ya Wabunge wetu Wapendwa.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Angekuwa wa ccm halafu ambaye yupo kwenye jimbo!!!! Du nisimalizie
   
 6. koo

  koo JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kapewa sum
   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  mkuu umeniacha hoi pamoja na kutokumalizia lakini nimekusoma vema
   
 8. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa uzoefu,vikao vya bunge huwa havipiti hivi hivi bila mtu kuded ama kuponea chupu chupu,bunge ni kuwa ni sawa na kijiji so matukio lazima yawepo.pole CUF na mheshimiwa, tatizo ndoa yenu inalegalega sana siku hizi hata huduma muhimu kwa bi CUF zimepungua sana tangu katoto kamezaliwa(ADC),ndoa kuvumilia!
   
 9. B

  Bem New Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umeona mbali sana
   
Loading...