PreGE2025 Mbunge Cicil Mwambe: Jimbo la Ndanda limetekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 85

PreGE2025 Mbunge Cicil Mwambe: Jimbo la Ndanda limetekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 85

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Mheshimiwa Cecil David Mwambe, amesema kuwa hadi kufikia sasa, utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 umefikia asilimia 85 katika jimbo hilo.

Akizungumza leo Mei 25, mbele ya mabalozi wa mashina wa CCM katika kikao maalum kilichofanyika Ndanda, Mwambe ametoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Ilani ya CCM.

Mbunge huyo ameeleza kwa fahari namna ambavyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imechangia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi hiyo.

“Tunaona mafanikio makubwa na ya wazi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji na miundombinu. Ni wazi kuwa kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Ndanda imeongezeka kwa kiwango kikubwa,” alisema Mwambe.

Akitolea mfano baadhi ya mafanikio hayo, Mwambe alisema miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, barabara, shule mpya pamoja na maboresho ya huduma ya maji vijijini imeleta mabadiliko chanya kwa wakazi wa Ndanda.

Mbunge huyo aliwashukuru wananchi wa Ndanda kwa ushirikiano wao na kuwataka kuendelea kuwa na imani na serikali ya CCM, akisisitiza kuwa maendeleo hayo ni ushahidi wa utekelezaji mzuri wa ahadi zilizotolewa katika kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020.

“Tunamshukuru kwa dhati Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake makini na maono ya maendeleo. Tumeshuhudia fedha nyingi zikitengwa na kutolewa kwa ajili ya kuleta huduma bora kwa wananchi wetu,” aliongeza.

Jimbo la Ndanda ni miongoni mwa majimbo yanayopokea kasi kubwa ya maendeleo katika Mkoa wa Mtwara, likiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha kuwa maendeleo yanawafikia wananchi wa pande zote za nchi.

 
Back
Top Bottom