Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Kahama, Emmanuel Cherehani amehoji utaratibu wa mgonjwa kulipia fedha ya kwenda kumuona daktari katika hospitali za Umma hapa nchini ambapo amedai wagonjwa hulipishwa kiasi cha shilingi 5,000 mpaka 30,000.
Soma pia: Dkt. Seif Shekalaghe: Marufuku hospitali kudai fedha kwa wagonjwa wa dharura kabla ya huduma
Cherehani ameuliza swali hilo hii leo Januari 29, 2026 wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu ambapo ameitaka serikali itoe kauli juu ya tozo hiyo ambayo imekuwa ikiwafanya wagonjwa kuteseka ilihali ya miundombinu kuboresha na madaktari kulipwa stahiki zao kutoka serikalini.
“Mheshmiwa Waziri Mkuu kumekuwa na malalamiko makubwa sana hapa nchini kwa Wananchi wetu wanaoenda kupata matibabu hospitali na zahanati zetu hata wakati mwingine kwenye Hospitali zetu zile za Rufaa wakifika wanaambiwa kutoa fedha za kumuona daktari maeneo mengine wanatozwa 5,000 mpaka 30,000 ilhali madaktari hawa ni waajiriwa wa Serikali wanalipwa na Serikali”
Akijibu swali hili Waziri Mkuu amesema “Mheshimiwa Spika kwa mujibu wa sheria ya bima ya afya kwa wote, utaratibu tulio jiwekea kama taifa kwenye maswala ya afya ni kuchangiana kwenye vitita mbalimbali ambavyo vinatolewa kama ambayo imeainishwa katika bima mbalimbali. Kwa wale ambao wanakuwa nje ya utaratibu wa bima ya Afya kwa wote ndio ambao wanakutana na changamoto ya kuchangia pale wanapofika katika hospitali zetu”
Hata hivyo Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Afya kuharakisha kutungwa kwa sheria ambayo itaweka viwango hivyo wanavyotozwa wagonjwa viwe sawa kwa nchi nzima badala ya kila eneo kuwa na utaratibu wake.