Mbunge CHADEMA atishiwa maisha, kisa fomu dhidi ya Mbowe

Nadhani ni dhahiri wako sahihi kabisa, ikibidi wafe kwa hofu na pressure zao hakuna wa kuwatisha.
Ccm mmewahujumu sana wabunge wa chadema kwa kuwanunua na wengine wana ushahidi wa kuwanunua tena kwa kuwatishia maisha wasipokubaliana.
Sasa hawataki watu wa kupewa dhamana kisha mkawanunua tulieni, waacheni wafanye chaguzi zao.
Sidhani kama kwenye chaguzi za Jafo waliwaingilia
 
Nilipofika tu hapa anasema Mchunganyi Munga Keason wa Kanisa la Fellowship nikaacha kusoma nikaendelea na shughuli zangu
Safari hii kuna wachungaji kadhaa, na makasisi wamesajiliwa kwenye kundinla wasiojulikana. Wengi ni hawa wanaoitwa makanisa ya kiroho.

Siongee kwa kufurahisha jukwaa, ninkwa uhakika japo siwezi kuweka vielelezo hapa. Na wanatoa taarifa kila siku kwa wakubwa zao. Na hao wachunguzeni, wenye akili mtawajua hao wasiojulikana wanaotumia makanisa na misikiti. Na waumini muwe makini katika kuyaweka wazi mambo yenu kwa viongozi wa dini, hasa wale mlio na mashaka nao.

Siku moja, kiongozi mmojawapo wa wasiojulikana, aliweka loudspeaker ya simu yake wakati akipokea taarifa toka kwa mtu anayejiita kiongozi wa kiroho, na akaniambia kuwa hakuna wakati ambao wasiojulikana wamekuwa na mtandao mpana kama awamu hii.
 
Kama ni kweli na inawezekana kabisa kuwa hivyo, basi hawa nao wanastahili kupelekwa huko SHENZISTAN. Mimi sioni ubaya wa Mbowe kuendelea lakini si kwa njia ya kutisha wanaotaka wagombee kiti hicho kikatiba. Haya ndio yanayotufanya tusiwe na vyama.
Katika maelezo yake, ulivyosoma, umeona mahali popote ambapo ameeleza ni vitisho gani vimetolewa? Vimetolewa na nani? Vimetolewa kwa njia gani?

Usipoteze muda kuziamini hizi hadithi za kijinga ambazo zipo kwaajili ya wajinga.

Ni vizuri kuwa na mabadiliko ya viongozi kila inapobidi na inapowezekana lakini siyo kwa propaganda za kiwendawazimu kama hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…