Mbunge auawa kwa kupigwa risasi Uganda

Mbunge auawa kwa kupigwa risasi Uganda

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
_101951291_aaa1c040-8192-4181-a806-0e27056dda7d.jpg

Mbunge wa Manispaa ya Arua nchini Uganda (MP), Ibrahim Abiriga ameuawa kwa kupigwa risasi karibu na nyumba yake huko Mattuga Wilaya ya Wakiso.

Alidaiwa kupigwa risasi na watu wawili waliokuwa wakiendesha boda boda mwendo wa saa kumi na mbili na nusu siku ya Ijumaa .

Mlinzi wake aliyekuwa akindamana naye pia alipigwa risasi katika gari lake.Alikuwa mmoja wa viongozi walioshinikiza kubadilishwa kwa katiba kuondoa kifungu cha 102b ili kuweza kuondoa kikomo cha umri wa rais cha miaka 75 kuondolewa.
Hatahivyo hatua yake ya kutaka kikomo hicho kuondolewa ilisitishwa na kesi mahakamani baada ya kutuhumiwa kukojoa katika eneo la umma karibu na makao makuu ya wizara ya fedha mjini kampala.
BBC
 
Apumzike kwa amani bwana Abiriga,mbele yake nyuma yetu.
 
Kuondoa kipengele cha umri tu katika katiba ya nchi ni adhabu ya kifo huko kwa wenzetu! Sijui ukigusa Maslahi ya Taifa na kuwa kibaraka adhabu yake ni nini?
Pumzika panapostahili bwana Abiriga.
 
Back
Top Bottom