Mbunge ataka wananchi waache tabia ya kuombaomba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge ataka wananchi waache tabia ya kuombaomba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kasheshe, Jan 14, 2009.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ally Sonda,Moshi

  MBUNGE wa Vunjo(CCM) Aloyce Kimaro amepiga marufuku tabia ya baadhi watu wa jimbo hilo kuishi maisha ya kuombaomba, badala yake amewataka wafanye kazi itakayowapatia kipato.

  Kimaro alisema hayo mwishoni mwa wiki,wakati wa uzinduzi wa Chama Cha Akiba na Mikopo Marangu cha UVIMA Saccos.

  Alisema watu wasiofanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri ni tatizo ndani ya jamii kwa vitendo vya kuomba na kukejeli shughuli zinazofanywa na Serikali,Wabunge na Madiwani.

  Mbunge huyo alisema maisha bora kwa kila mtanzania hayamfuati mtu aliyejipumzisha baa au kwenye klabu cha pombe au anayelalamikia serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Akizungumzia uzinduzi wa Saccos hiyo Kimaro alivitaka vikundi vya benki kata kwenye jimbo la Vunjo (VICOBA) kushirikiana ili vifanikishe malengo ya kuwasaidia wananchi kupambana na umasikini.

  "Akina mama zangu, na ndugu zangu wote wa Vunjo,hakuna mtu atakaewaletea maendeleo hapa bila ninyi kujikwamua kwanza, hakikisheni Vicoba na Saccos mlizoanzisha mnazilinda na mpendane na kuaminiana,"alisema Kimaro.

  Katika uzinduzi wa Saccos hiyo, uliofanywa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi,Kimaro aliahidi kutoa tani 2.5 za mbolea ya minjingu na kiasi kingine cha Sh.1 milioni ili kusaidia wananchi.

  Viongozi wengine waliochangia Saccos hiyo ili iweze kujiendeleza ni Mengi aliyetoa Sh.50 milioni na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa,Crispin Meela aliyechangia Sh.500,000.

  Zaidi ya Sh. Milioni 70 zilipatikana katika hafla hiyo.  -------------------------------------------------------------------------------------------------------
  Tunahitaji viongozi wengi wanaohamasisha wananchi kufanya kazi, kwa ajili ya maendeleo ya taifa, viongozi wa namna hii hivi sasa ni wachache sana... hapa ndio namkumbuka Mh. Edward Lowassa maana yeye alikuwa anasema wazi kwamba maisha bora yanaletwa na kufanya kazi.... sasa hivi sisikii tena viongozi wakihamasisha ufanyaji kazi tena kwa bidii na maarifa.

  Nachukia viongozi wanaowaambiwa wananchi kwamba wao(viongozi) ndio wanaoweza kuwaletea maendeleo wananchi...

  Viongozi wa namna hiyo ndio wanaodumaza uchumi wa nchi....
   
 2. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ombaomba wapo wa ngazi nyingi tuu, Hata viongozi wa nchi huenda nje kuomba misaada. Cha msingi wananchi wawezeshwe ili wajiajili siyo kuwasema tuu na hali mali asili zetu (madini/migodi) ambazo zingetusaidia wananchi mmezimilikisha kwa makaburu, na kuwaruhusu watuue endapo tunasogea huko.
   
Loading...